The chat will start when you send the first message.
1Jina zuri ni jema kuliko mafuta mazuri, nayo siku ya kufa ni njema kuliko siku ya kuzaliwa.[#Fano. 22:1.]
2Kuingia nyumbani mwenye matanga ni kwema kuliko kuingia nyumbani mwenye watu wanywao, kwa kuwa mle huelekea mwisho wa watu wote, naye mwenye uzima huyaweka moyoni.
3Masikitiko ni mema kuliko macheko, kwani uso ukiwa mbaya, moyo huwa mwema.
4Mioyo ya werevu wa kweli huwa nyumbani mwenye matanga, lakini mioyo ya wajinga huwa nyumbani mwenye furaha.
5Kuyasikiliza makemeo ya mwerevu wa kweli ni kwema, kuliko mtu akizisikiliza nyimbo za wajinga.
6Kwani kama moto wa miiba unavyovuma chini ya chungu, ndivyo, macheko ya mjinga yalivyo; hayo nayo ni ya bure.
7Kweli ukorofi humpumbaza mwerevu wa kweli, nayo mapenyezo huzipoteza akili.
8Mwisho wa jambo ni mwema kuliko mwanzo wake; mwenye uvumilivu ni mwema kuliko mwenye majivuno.
9Usiwe mwepesi wa kukasirika rohoni mwako; kwani makasiriko hutua kufuani mwa mjinga.[#Yak. 1:19.]
10Usiulize kwamba: Inakuwaje, siku za kale zikiwa njema kuliko hizi za sasa? Kwani huulizi hivyo kwa kuwa mwenye werevu wa kweli.
11Werevu wa kweli ni mwema kama fungu uliloachiwa, tena ni pato kwao walionao jua.
12Kivulini kwa werevu wa kweli ni kuzuri kama kivulini kwa fedha, lakini ujuzi hushinda, kwa kuwa werevu wa kweli huwapatia wenyewe uzima.[#Fano. 3:2.]
13Yatazame matendo yake Mungu! Kwani yuko nani awezaye kuyanyosha aliyoyapotoa?[#Mbiu. 1:15.]
14Siku ikiwa njema, nawe furahiwa! Lakini siku ikiwa mbaya, jiangalie! Kwani hii nayo Mungu ameifanya, kama alivyoifanya ile, kwa kwamba: Mtu asione cho chote kitakachokuwako nyuma yake.
15Haya yote mawili niliyaona katika siku zangu zilizo za bure nazo: wako waongofu wanaoangamia, ijapo wawe wenye wongofu, tena wako wasiomcha Mungu wanaokaa siku nyingi, ijapo wawe wenye ubaya.[#Mbiu. 8:14; Sh. 73:12-13.]
16Usiuzidishe wongofu, wala usijipatie werevu wa kweli kushinda wengine! Kwa nini unataka kujiangamiza?
17Tena usizidishe uovu, wala usiwe mjinga! Kwa nini unataka kufa, siku zako zikiwa hazijatimia bado?
18Ni vema, ushike upande huu! Lakini napo penye upande mwingine usiuondoe mkono wako! Kwani amchaye Mungu huyapona yote mawili.
19Werevu wa kweli humtia mwerevu wa kweli nguvu zaidi kuliko wakuu kumi watawalao mjini.
20Kwani huku nchini hakuna mtu mwongofu afanyaye mema tu pasipo kukosa.[#Sh. 14:3.]
21Tena usiyaangalie maneno yote, watu wanayoyasema, usije kumsikia mtumishi wako, akikutukana!
22Kwani moyo wako unajua, ya kuwa nawe mara nyingi ulitukana wengine.
23Hayo yote niliyajaribu kwa werevu wa kweli, nikasema: Na nierevuke kweli! Lakini werevu wa kweli hunikalia mbali.
24Iliyokuwa sababu yao ya kuwa hivyo iko mbali, tena imefichika sanasana, atakayeivumbua yuko nani?
25Nikazunguka, moyo wangu upate ujuzi na uchunguzi kwa kuutafuta werevu wa kweli na utambuzi, ujue, ya kuwa kumwacha Mungu ni ujinga, nao ujinga ndio upumbavu.
26Ndipo, nilipoona yaliyo yenye uchungu kuliko kufa, ndio mwanamke, moyo wake ukigeuka kuwa tanzi na wavu, nayo mikono yake ikiwa pingu. Mtu aliye mwema machoni pake Mungu huponyoka kwake, lakini mkosaji hunaswa naye.[#Fano. 2:16-22.]
27Mpiga mbiu akasema: Yatazame, niliyoyaona kwa kuunganisha moja kwa moja, nipate kuyatambua yaliyo kweli!
28Liko moja, roho yangu ililolitafuta pasipo kuliona: Mwanamume nimemwona mmoja katika elfu, lakini mwanamke, niliyemtafuta, sikumwona katika wao wote.
29Lakini hili moja, nililoliona, litazame nalo: Mungu alimwumba mtu kuwa mwongofu, lakini wao hutafuta mizungu mingi![#Fano. 2:7.]