The chat will start when you send the first message.
1Saa ile wanafunzi wakamjia Yesu, wakamwuliza wakisema: Aliye mkuu katika ufalme wa mbingu ni nani?
2Akaita kitoto, akamsimamisha katikati yao,
3akasema: Kweli nawaambiani: Msipogeuka, mkawa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbingu.[#Mat. 19:14; Yoh. 3:3,5.]
4Mtu atakayejinyenyekeza mwenyewe, awe kama kitoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbingu.
5Naye atakayepokea kitoto mmoja kama huyu kwa jina langu hunipokea mimi.[#Mat. 10:40; Yoh. 13:20.]
6Lakini mtu atakayekwaza mmoja tu aliye mwenzao hawa wadogo wanaonitegemea inamfaa kutungikwa shingoni pake jiwe kubwa la kusagia, kisha atoswe kilindini mwa bahari.[#Luk. 17:1-2.]
7Yako yatakayoupata ulimwengu kwa ajili ya makwazo. Kweli makwazo sharti yaje, lakini mtu yule anayelileta kwazo atapatwa na mambo.[#Mat. 16:23.]
8Nawe, mkono wako ukikukwaza, au mguu wako ukikukwaza, uukate uutupe mbali! Kuingia penye uzima mwenye kilema au kiwete kutakufaa kuliko hapo, ukiwa mwenye mikono miwili au miguu miwili, ukatupwa katika moto usiozimika kale na kale.[#Mat. 5:29-30.]
9Nalo jicho lako likikukwaza, basi ling'oe ulitupe mbali! Kuingia penye uzima mwenye chongo kutakufaa kuliko hapo, ukiwa mwenye macho mawili, ukatupwa shimoni mwa moto.
10Tazameni, msiwabeze wadogo hawa hata mwenzao mmoja! Kwani nawaambiani: Malaika zao mbinguni huutazama siku zote uso wa Baba yangu alioko mbinguni.[#Ebr. 1:14.]
11Kwani Mwana wa mtu amekuja kukiokoa kilichoangamia.[#Mat. 9:13; Luk. 19:10.]
(12-14: Luk. 15:4-7.)12Mwaonaje? Mtu akiwa na kondoo mia, tena mmoja wao akipotea, hatawaacha wale tisini na tisa milimani, aende kumtafuta yule aliyepotea?
13Naye akipata kumwona, kweli nawaambiani: Atamfurahia kuliko wale tisini na tisa wasiopotea.
14Vivyo hivyo Baba yenu alioko mbinguni hataki, hawa walio wadogo hata mmoja wao apotee.
15Ndugu yako akikukosea, nenda kamwonye, wewe na yeye mko peke yenu! Akikusikia, umempata tena ndugu yako.[#3 Mose 19:17; Luk. 17:3-4; Gal. 6:1.]
16Lakini asipokusikia, chukua pamoja na wewe tena mmoja au wawili! Maana kila shauri limalizike kwa kusemewa na mashahidi wawili au watatu.[#5 Mose 19:15.]
17Naye akikataa kuwasikia hao, waambie wateule wenziwe shauri hilo! Lakini atakapokataa kuwasikia nao wateule, awe kwako kama mtu wa kimizimu au mtoza kodi![#1 Kor. 5:13; 2 Tes. 3:6; 1 Tim. 6:4-5; Tit. 3:10.]
18Kweli nawaambiani: Lo lote, mtakalolifunga nchini, litakuwa limefungwa hata mbinguni; nalo lo lote, mtakalolifungua nchini, litakuwa limefungwa hata mbinguni; nalo lo lote, mtakalolifungua nchini, litakuwa limefunguliwa hata mbinguni.[#Mat. 16:19; Yoh. 20:23; Tume. 15:28-30; 1 Kor. 5:4-5.]
19Tena nawaambiani: Kila jambo, wenzenu wawili nchini watakalopatana kuliomba, watapewa na Baba yangu alioko mbinguni.[#Mar. 11:24.]
20Kwani watu wawili au watatu wanapolikusanyikia Jina langu, nami nipo hapo katikati yao.[#Mat. 28:20; Yoh. 14:23.]
21*Ndipo, Petero alipomjia, akamwambia: Bwana, ndugu yangu anikosee mara ngapi, nikimwondolea? Yatosha mara saba?
22Yesu akamwambia: Sikuambii: Mwondolee mara saba, ila mwondolee mara sabini mara saba![#Luk. 17:4; Ef. 4:32.]
23Kwa sababu hiyo ufalme wa mbingu umefanana na mfalme aliyetaka kufanya hesabu na watumwa wake.
24Alipoanza kuhesabu akaletewa mmoja mwenye madeni ya mizigo 10000 ya fedha.
25Naye alipokosa vya kumlipa, bwana akaagiza, wauzwe yeye na mkewe na watoto wake navyo vyote, alivyokuwa navyo, deni lipate kulipika.
26Mtumwa akamwangukia, akamlalamikia akisema: Nivumilie, nitakulipa yote!
27Bwana akamwonea uchungu yule mtumwa, akamfungua, akamwachilia hata deni lake.
28Lakini yule mtumwa alipotoka akamwona mtumwa mwenziwe mmoja aliyekuwa mdeni wake wa shilingi 100. Akamkamata, akamshika koo, akasema: Lipa deni lako!
29Mtumwa mwenziwe akaanguka miguuni pake, akambembeleza akisema: Nivumilie, nitakulipa!
30Lakini yule hakutaka, akaenda, akamtia kifungoni, mpaka atakapolilipa lile deni.
31Basi, watumwa wenziwe walipoyaona yaliyokuwa wakasikitika sana. Wakaja, wakamweleza bwana wao hayo yote yaliyokuwa.
32Ndipo, bwana wake alipomwita, akamwambia: Wee mtumwa mbaya, lile deni lote nalikuachilia, uliponibembeleza.
33Wewe nawe haikukupasa kumhurumia mtumwa mwenzio, kama nilivyokuhurumia mimi?
34Bwana wake akakasirika, akamtoa, afungwe, mpaka atakapolilipa deni lake lote.[#Mat. 5:26; Yak. 2:13.]
35Ndivyo, naye Baba yangu wa mbinguni atakavyowatendea ninyi, msipoondoleana mioyoni mwenu kila mtu na ndugu yake.*[#Mat. 6:14-15.]