The chat will start when you send the first message.
1Hivyo mlivyo naye Kristo, nawabembeleza kwamba: Ikiwa mwatulizana mioyo kwa kupendana, ikiwa m wenye roho moja, au ikiwa m wenye mioyo ya kuoneana uchungu na huruma,
2ikiwa hivyo, itimilizeni furaha yangu, mawazo yenu yakiwa yayo hayo ya kupendana kila mtu na mwenziwe, mioyo ikiwa mmoja tu wa kulitaka neno lili hili la kwamba:
3Pasifanyike jambo lolote kwa kuchokozana wala kwa kujitakia majivuno ya bure, ila mnyenyekeane kila mtu akimwazia mwenziwe kuwa mkubwa kuliko yeye![#Rom. 12:10; Gal. 5:26.]
4Kila mtu asiyaangalie yaliyo yake tu, ila na ayaangalie nayo yaliyo yake mwenziwe!*[#1 Kor. 10:24,33.]
5*Mioyoni mwenu myawaze yaleyale, Kristo Yesu aliyoyawaza![#Mat. 11:29.]
6Yeye alikuwa mwenye sura yake Mungu, tena kule kufanana naye Mungu hakushikamana nako kama ni kitu, alichokiponyoka.[#1 Mose 3:5; Yoh. 1:1-2; 17:5.]
7Ila alijivua mwenyewe sura ya Kimungu, akajivika sura ya kitumwa, akawa amefanana na watu; walipomtazama, akaonekana, kuwa kama mtu mwenyewe.[#Yes. 53:3; 2 Kor. 8:9; Ebr. 2:14,17.]
8Akajinyenyekeza mwenyewe, akawa mwenye kutii mpaka kufa, kweli mpaka kufa msalabani.[#Ebr. 12:2; 5:8.]
9Kwa hiyo naye Mungu alimkweza mbinguni, akampatia Jina lililo kuu kuliko majina yote,[#Tume. 2:33; Ef. 1:21; Ebr. 1:3-4.]
10maana katika Jina lake Yesu wote wapige magoti, wao walioko mbinguni nao waliopo nchini nao walioko kuzimuni,[#Yes. 45:23; Yoh. 5:23; Ufu. 5:13.]
11kila ulimi uungame kwamba: BWANA ni YESU KRISTO; hivyo ndivyo, naye Mungu Baba atakavyotukuzwa.*
12Wapenzi wangu, kama mlivonitii siku zote, ikiwa niko kwenu, hata ikiwa siko kama siku hizi za sasa: Usumbukieni wokovu wenu wenyewe mkitetemeka kwa kuogopa![#Sh. 2:11; 1 Petr. 1:17.]
13Kwani Mungu ndiye aliyewapa kwanza mioyo ya kutaka, kisha ndiye atakaye wapa nako kuyamaliza yampendezayo.[#Yoh. 15:5; 2 Kor. 3:5.]
14Yote yafanyeni pasipo kunung'unika na pasipo kuwaza mengi,[#1 Petr. 4:9.]
15mtu asione la kuwaonya, mkiwa wenye hilo Neno moja tu! Hivyo mtakuwa wana wa Mungu wakaao pasipo kilema katikati yao wa ukoo huu wenye uangamizi na upotovu. Katikati yao ndiko, mnakoangaza, kama mianga inavyoangaza ulimwenguni,[#Fil. 1:10; Mat. 5:14; 10:16; Ef. 5:8.]
16mkilishika Neno la uzima; hivyo nami nitapata majivuno siku ya Kristo kwamba: Sikupiga mbio bure, wala sikusumbuka bure.[#Yes. 49:4; Gal. 2:2; 1 Tes. 2:19.]
17Lakini hata nikiuawa kama ng'ombe ya tambiko, ikiwa ya kuwatumikia tu, nafurahi na kuwafurahisha nanyi nyote.[#Kol. 1:24; 2 Tim. 4:6.]
18Vivi hivi hata ninyi furahini na kunifurahisha nami![#Fil. 3:1; 4:4.]
19Namngojea Bwana Yesu, aitikie, nimtume Timoteo upesi kwenu, moyo wangu upate kutulia ukitambua, mambo yenu yalivyo.
20Kwani sinaye mtu mwingine, tuliyepatana naye mioyo kama huyu; naye huyasumbukia kweli mambo yenu.[#1 Kor. 16:10.]
21Kwani wote huyafuata yaliyo yao; hawayafuati yaliyo yake Kristo Yesu.[#2 Tim. 4:10,16.]
22Lakini yeye mmemtambua, ya kuwa ni mwelekevu, kwani kama mtoto anavyomtumikia baba yake, vivyo hivyo ameitumikia kazi ya kuutangaza Utume mwema pamoja nami.
23Nangojea, nipate kumtuma yeye; itakuwa papo hapo, nitakapoona, mambo yangu yatakavyotimilika.[#Fil. 1:12.]
24Hili nalo nalishika moyoni kwamba: Bwana atanipa nami kuja upesi kwenu.[#Fil. 1:25.]
25Lakini nalishurutishwa moyoni kumtuma Epafurodito kwenu; yeye ni ndugu na mwenzangu wa kazi na wa vita; kisha ni mtume wenu anayenipatia yenye kunitunza.[#Fil. 4:18.]
26Akawa akiwatunukia ninyi nyote, akasikitika sana, kwa sababu mlikuwa mmesikia, ya kuwa aliugua.
27Naye alikuwa mgonjwa kweli, kufa kukamfikia. Lakini Mungu akamhurumia, tena siye yeye tu, ila mimi nami, masikitiko yasifuatane kwangu mimi.
28Kwa hiyo nimemtuma upesiupesi, mpate kuonana naye na kufurahi tena, nami masikitiko yanipungukie.
29Kwa hiyo mpokeeni katika Bwana kwa furaha yote! Nao walio hivyo wapeni macheo![#1 Kor. 16:16.]
30Kwani kwa ajili ya kazi ya Kristo alijifikisha kufani, asijitunzie mwenyewe, akitaka kunifanyizia kazi zote za utumishi, ambazo hamkuweza kunifanyizia.