The chat will start when you send the first message.
1Mbona wamizimu hupiga makelele? Mbona makabila ya watu huwaza mambo yaliyo ya bure?[#Tume. 4:25-30.]
2Wafalme wa nchi hushikana mioyo, wakuu nao hula njama wakikaa pamoja, wamkatae Bwana na Masiya wake kwamba:[#Ufu. 11:18; 19:19.]
3Na tuyavunje mafungo yao! na tuzitupe kamba zao, zisitufunge tena![#Yer. 2:20; 5:5; Luk. 19:14.]
4Lakini akaaye mbinguni anawacheka, yeye Bwana anawafyoza.[#Sh. 37:13; 59:9.]
5Siku zitakapotimia, atasema nao kwa makali yake, awastushe kwa moto wa machafuko yake:[#Yes. 34; Ufu. 6:15-17.]
6Mimi nimemsimika mfalme wangu huko mlimani kwa Sioni kwenye utukufu wangu.
7Nitasimulia shauri, Bwana aliloniambia: Wewe ndiwe Mwanangu, siku hii ya leo mimi nimekuzaa.[#2 Sam. 7:14; Sh. 89:27-30; Tume. 13:33; Ebr. 1:5; 5:5.]
8Omba kwangu! Nami nitakupa wamizimu, wawe fungu lako, nayo mapeo ya nchi, yawe mali zako![#Dan. 7:13-14; Ebr. 1:2.]
9Kwa fimbo ya chuma utawaponda, kama vyombo vya mfinyanzi utawavunja.[#Ufu. 2:27; 12:5; 19:15.]
10Sasa nyie wafalme, pambanukeni! Nanyi waamuzi wa nchi, onyekani!
11Mtumikieni Bwana kwa kumwogopa! Mshangilieni kwa kutetemeka![#Fil. 2:12; Ebr. 12:28.]
12Mnoneeni Mwana, asiwatolee makali, mkaangamia njiani! Maana moto wa makali yake utawaka upesi. Wenye shangwe ndio wote wamwegemeao![#1 Sam. 10:1; Sh. 34:9; 84:13; Yes. 30:18; Yoh. 3:36.]