The chat will start when you send the first message.
1Ninapokulilia, niitikie, Mungu unipaye wongofu! Hunipatia mahali pakubwa, nikiwa nimesongwa; sasa nihurumie na kuyasikia maombo yangu!
2Ninyi wana wa watu mpendao mambo ya bure, mpaka lini mwanitia soni na kuninyima heshima, mpaka lini mtayanyatia yaliyo uwongo tu?
3Lakini tambueni, ya kuwa Bwana humkuza amchaye! Bwana hunisikia, kila ninapomlilia.[#Sh. 17:7.]
4Stukeni, msije kukosa! Semeni mioyoni mwenu, mnapolala, mpate kutulia![#Sh. 16:7; Ef. 4:26.]
5Tambikeni na kutoa vipaji vya tambiko vyenye wongofu, nanyi mpate kumwegemea aliye Bwana![#Sh. 51:19,21; 1 Petr. 2:5.]
6Wako wengi wanaosema kwamba: Yuko nani atakayetuonyesha kilicho chema? Bwana, utokeze mwanga wa uso wako, uwe juu yetu![#4 Mose 6:25-26.]
7Umenipa furaha moyoni mwangu ipitayo yao ya kufurikiwa na vyakula na vinywaji.
8Hivyo nitalala usingizi na kutengemana pia, kwani wewe ndiwe Bwana peke yako, unanipatia makao yasiyoshindika.[#Sh. 3:6; 3 Mose 26:6.]