The chat will start when you send the first message.
1Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi.[#Rum 2:1; 1 Kor 4:5]
2Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa.[#Mk 4:24]
3Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huioni?
4Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe?
5Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.
6Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua.[#Mt 10:11]
7Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;[#Mk 11:24; Lk 11:9-13; Yer 29:13,14; Yn 14:13; 16:23]
8kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.
9Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe?
10Au akiomba samaki, atampa nyoka?
11Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu zawadi njema, je! Si Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema zaidi wao wamwombao?[#Yak 1:17]
12Basi yoyote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo Torati na Manabii.[#Lk 6:31; Mt 22:39,40; Rum 13:8-10]
13Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.[#Lk 13:24; Yn 10:7,9]
14Bali mlango ni mwembamba, na njia imebana iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.[#Mt 19:24; Mdo 14:22]
15Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wakiwa wamevaa mavazi ya kondoo, lakini kwa ndani ni mbwamwitu wakali.[#Mt 24:4,5,24; Mdo 20:29]
16Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?[#Gal 5:19-22; Yak 3:12]
17Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya.[#Mt 12:33]
18Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri.
19Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni.[#Mt 3:10; Lk 3:9; Yn 15:2,6]
20Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.[#Mt 12:33]
21Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.[#Mt 21:29; Rum 2:13; Yak 1:22,25; 2:14; 1 Kor 12:3]
22Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?[#Yer 14:14; 27:15; Lk 13:25-27; 1 Kor 13:1,2]
23Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.[#Zab 6:9; Mt 13:41; 25:41; 2 Tim 2:19]
24Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;[#Mt 7:21]
25mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba.
26Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga;
27mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.[#Eze 13:10,11]
28Ikawa, Yesu alipoyamaliza maneno hayo, makutano walishangaa mno kwa mafundisho yake;[#Mk 1:22; Lk 4:32; Mt 11:1; 13:53; 19:1; 26:1]
29kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye mamlaka, wala si kama waandishi wao.[#Yn 7:46]