The chat will start when you send the first message.
1Kisha BWANA akanena na Musa katika bara ya Sinai, mwezi wa kwanza wa mwaka wa pili baada ya kutoka kwao katika nchi ya Misri, akamwambia,[#Kut 12:1-13]
2Tena, wana wa Israeli na waadhimishe sikukuu ya Pasaka kwa wakati wake ulioagizwa.[#Kut 12:1; Law 23:5; Kum 16:1,2; Hes 28:16; Ebr 10:1]
3Siku ya kumi na nne ya mwezi huu, wakati wa jioni, mtaiadhimisha kwa wakati wake ulioagizwa; kwa amri zake zote, na kama hukumu zake zote zilivyo, ndivyo mtakavyoisherehekea.
4Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli kwamba waadhimishe sikukuu hiyo ya Pasaka;
5Nao wakaiadhmisha Pasaka katika mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni, katika bara ya Sinai vile vile kama hayo yote BWANA aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyofanya wana wa Israeli.[#Yos 5:10]
6Basi walikuwako wanaume kadhaa waliokuwa na unajisi kwa ajili ya maiti wa mtu, hata wasiweze kuishika Pasaka siku hiyo; nao wakaenda mbele ya Musa na Haruni, siku hiyo hao watu wakamwambia,[#Hes 5:2; 6:6,7; Yn 18:28; Kut 18:15; Hes 27:2]
7Sisi tuko katika hali ya unajisi kwa ajili ya maiti wa mtu; nasi tumezuiwa kwa nini hata tusipate kumtolea BWANA matoleo kwa wakati wake ulioagizwa, kati ya wana wa Israeli?[#1 Kor 5:7,8]
8Musa akawaambia, Ngojeni hapo; hata nipate sikiza BWANA atakaloagiza juu yenu.[#Zab 25:14; 85:8; Yn 7:17; Efe 1:9,18; Ebr 3:5,6]
9BWANA akanena na Musa, akamwambia,
10Nena na wana wa Israeli, kuwaambia, Mtu wa kwenu, au wa vizazi vyenu, yeyote atakayekuwa na unajisi kwa ajili ya maiti, au akiwako mbali katika safari, na haya yote, ataishika Pasaka kwa BWANA;
11mwezi wa pili, siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni, wataishika; watamla pamoja na mikate isiyotiwa chachu na mboga za uchungu;[#2 Nya 30:2,15; Kut 12:8; #9:11 Katika Kiebrania ni ‘katikati ya jioni’.]
12wasisaze kitu chake chochote hadi asubuhi, wala wasimvunje mfupa wake; kama hiyo sheria yote ya Pasaka ilivyo ndivyo watakavyoishika.[#Kut 12:10,43,46; Yn 19:36]
13Lakini mtu aliye safi, wala hakuwa katika safari, naye amekosa kuishika Pasaka, mtu huyo atatengwa na watu wake; kwa sababu hakumtolea BWANA matoleo kwa wakati wake ulioamriwa, mtu huyo atachukua dhambi yake.[#Mwa 17:14; Kut 12:15; Law 17:4; Ebr 6:6; 12:25; Hes 5:31; Gal 3:10; Ebr 10:26]
14Na kama mgeni akiketi kati yenu ugenini, naye ataka kuishika Pasaka kwa BWANA; kama hiyo sheria ya Pasaka ilivyo, na kama amri yake ilivyo, ndivyo atakavyofanya; mtakuwa na sheria moja, kwa huyo aliye mgeni, na kwa huyo aliyezaliwa katika nchi.[#Kut 12:49]
15Na siku hiyo maskani iliposimamishwa, lile wingu likaifunika maskani, yaani, hema ya kukutania; wakati wa jioni likawa juu ya maskani, mfano wa moto, hata asubuhi.[#Kut 13:21]
16Ndivyo ilivyokuwa sikuzote; lile wingu liliifunika kwa mfano wa moto usiku.[#Kut 13:21,22; 40:34; Kum 1:33; Neh 9:12]
17Na kila lilipoinuliwa lile wingu juu ya ile Hema ndipo wana wa Israeli waliposafiri; na mahali lilipokaa lile wingu, ndipo wana wa Israeli walipopiga kambi yao.[#Kut 40:36,37; Hes 10:11,33,34; Zab 78:14; 80:1; Isa 49:10; Yn 10:4]
18Kwa amri ya BWANA Wana wa Israeli walisafiri, na kwa amri ya BWANA walipiga kambi; wakati lile wingu ilipokaa juu ya maskani walikaa katika kambi yao.[#1 Kor 10:1]
19Hata lile wingu lilipokawia juu ya maskani siku nyingi, wana wa Israeli walimtii BWANA, na hawakusafiri.
20Na pengine lile wingu lilikaa juu ya maskani siku chache; ndipo kwa amri ya BWANA walikaa katika kambi yao, tena kwa amri ya BWANA walisafiri.[#Zab 48:14; Mit 3:5,6]
21Na pengine lile wingu lilikaa tangu jioni hata asubuhi; na lile wingu lilipoinuliwa asubuhi walisafiri, au kama likikaa usiku na mchana pia, lilipoinuliwa lile wingu, ndipo waliposafiri.[#Mt 28:20]
22Ikiwa lile wingu lilikawia, likikaa juu ya maskani siku mbili, au mwezi, au mwaka, wana wa Israeli walikaa katika kambi yao, wasisafiri;[#Kut 40:36,37; Zab 73:24; 107:7; Isa 63:14]
23bali lilipoinuliwa walisafiri. Kwa amri ya BWANA walipiga kambi yao, na kwa amri ya BWANA walisafiri; walimtii BWANA, kwa mkono wa Musa.[#Zab 73:24; 107:7; Isa 63:14]