The chat will start when you send the first message.
1Mshangilieni BWANA, enyi nchi zote;
2Mtumikieni BWANA kwa furaha;
Njoni mbele zake mkiimba;
3Jueni kwamba BWANA ndiye Mungu;[#Ayu 10:8,9; Mhu 12:1; Efe 2:10; Eze 34:30]
Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake;
Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake.
4Ingieni malangoni mwake kwa shukrani;
Nyuani mwake kwa kusifu;
Mshukuruni, lihimidini jina lake;
5Maana BWANA ni mwema;[#1 Nya 16:34; 2 Nya 5:13; 7:3; Ezr 3:11; Zab 106:1; 107:1; 118:1; 136:1; Yer 33:11]
Rehema zake ni za milele;
Na uaminifu wake katika vizazi vyote.