Zaburi 110

Zaburi 110

Hakikisho la ushindi kwa mteule wa Mungu

1Neno la BWANA kwa Bwana wangu,[#Zab 45:6; Mt 22:44; Mk 12:36; Lk 20:42-43; 1 Kor 15:25; Mdo 2:34-35; 1 Kor 15:25; Efe 1:20-22; Kol 3:1; Ebr 1:13; 8:1; 10:12-13]

Uketi upande wangu wa kulia,

Hadi niwafanyapo adui zako

Kuwa chini ya miguu yako.

2BWANA atainyosha toka Sayuni

Fimbo ya nguvu zako.

Uwe na enzi kati ya adui zako;

3Watu wako watajitoa kwa hiari,[#Amu 5:2; Zab 96:9; Mdo 2:41]

Siku ya uwezo wako;

Kwa uzuri wa utakatifu,

Tokea tumbo la asubuhi,

Unao umande wa ujana wako.

4BWANA ameapa,[#Hes 23:19; Zek 6:13; Ebr 5:6; 6:20; 7:17,21]

Wala hataghairi,

Ndiwe kuhani hata milele,

Kwa mfano wa Melkizedeki.

5Bwana yu mkono wako wa kulia;[#Zab 16:8; 2:5; Rum 2:5; Ufu 11:18]

Atawaponda wafalme,

Siku ya ghadhabu yake.

6Atahukumu kati ya mataifa,[#Hab 3:13]

Ataijaza nchi mizoga;

Atawaponda wakuu katika nchi nyingi.

7Atakunywa maji ya mto njiani;[#Isa 61:1; Yn 3:34; Isa 53:12]

Kwa hiyo atakiinua kichwa chake kwa ushindi.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Published by: Bible Society of Kenya