Zaburi 120

Zaburi 120

Sala ya ukombozi

1Katika shida yangu nilimlilia BWANA

Naye akaniitikia.

2Ee BWANA, uniponye

Na midomo ya uongo na ulimi wa hila.

3Akupe nini, akuzidishie nini,

Ewe ulimi wenye hila?

4Mishale ya mtu hodari iliyochongoka,

Pamoja na makaa ya mretemu.

5Ole wangu mimi![#Mwa 10:2; 1 Sam 25:1; Yer 49:28]

Kwa kuwa ni mgeni katika Mesheki;

Na kufanya makao yangu

Katikati ya hema za Kedari.

6Kwa muda mrefu nimeishi,

Pamoja na watu wanaoichukia amani.

7Mimi nazingatia amani;

Bali ninenapo, wao wanataka vita.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Published by: Bible Society of Kenya