The chat will start when you send the first message.
1Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu,[#Eze 23:3; Hos 2:15]
Israeli na aseme sasa,
2Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu,
Lakini hawakuniweza.
3Wakulima wamelima mgongoni mwangu,[#Ebr 11:36]
Wamefanya mirefu mifuo yao.
4BWANA ndiye mwenye haki,[#2 The 1:6]
Amezikata kamba zao wasio haki.
5Na waaibishwe, warudishwe nyuma,
Wote wanaoichukia Sayuni.
6Na wawe kama majani ya darini[#Zab 37:2; Yer 17:5-6]
Yanyaukayo kabla hayajamea.
7Ambayo mvunaji haujazi mkono wake,
Wala mfunga miganda kifua chake.
8Wapitao nao hawasemi, Amani ya BWANA ikae nanyi,[#Rut 2:4; Zab 118:26]
Twawabariki kwa jina la BWANA.