Zaburi 2

Zaburi 2

Ahadi ya Mungu kwa mtiwa mafuta wake

1Mbona mataifa yanafanya ghasia,[#Mdo 4:25-26]

Na watu kuwaza mambo ya bure?

2Wafalme wa dunia wanajipanga,[#Zab 45:7; Yn 1:41]

Na wakuu wanafanya shauri pamoja,

Juu ya BWANA,

Na juu ya masihi wake,

3Na tuvipasue vifungo vyao,[#Lk 19:14]

Na kuzitupa mbali nasi kamba zao.

4Yeye aketiye mbinguni anacheka,[#Zab 11:4]

Bwana anawafanyia dhihaka.

5Ndipo atakaposema nao kwa hasira yake,

Na kuwafadhaisha kwa ghadhabu yake, akisema:

6Nami nimemweka mfalme wangu

Juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.

7Nitaihubiri amri; BWANA aliniambia,[#Mdo 13:33; Ebr 1:5; 5:5; Mt 8:29]

Wewe ni mwanangu, Mimi leo nimekuzaa.

8Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako,[#Dan 7:13,14; Yn 17:4,5]

Na miisho ya dunia kuwa milki yako.

9Utawaponda kwa fimbo ya chuma,[#Ufu 2:26-27; 12:5; 19:15; Mt 21:44]

Na kuwavunja kama chombo cha mfinyanzi.

10Na sasa, enyi wafalme, iweni na hekima,

Enyi watawala wa dunia, mwaonywa.

11Mtumikieni BWANA kwa kicho,

Shangilieni kwa kutetemeka.

12Shikeni yaliyo bora, asije akafanya hasira[#Yn 5:22,23; Yer 17:7; #2:12 Au, Pokeeni mafundisho au, Mbu suni Mwana.]

Nanyi mkapotea njiani,

Kwa kuwa hasira yake huwaka upesi;

Heri wote wanaomkimbilia.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Published by: Bible Society of Kenya