The chat will start when you send the first message.
1BWANA akujibu siku ya dhiki,[#Isa 50:10]
Jina la Mungu wa Yakobo likuinue.
2Akutumie msaada toka patakatifu pake,
Na kukutegemeza toka Sayuni.
3Azikumbuke sadaka zako zote,
Na kuzitakabali dhabihu zako.
4Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako,[#1 Yoh 5:14,15]
Na kukutimizia mipango yako yote.
5Na tuushangilie wokovu wako,[#Isa 12:1,2; 1 Sam 17:45]
Kwa jina la Mungu wetu tuzitweke bendera zetu.
BWANA akutimizie matakwa yako yote.
6Sasa najua kuwa BWANA amwokoa masihi wake;[#20:6 Au, mtiwa mafuta.]
Atamjibu toka mbingu zake takatifu,
Kwa matendo makuu ya wokovu
Ya mkono wake wa kulia.
7Hawa wanataja magari na hawa farasi,[#Amu 7:7]
Lakini sisi tutalitaja jina la BWANA, Mungu wetu.
8Wao wameinama na kuanguka,
Bali sisi tumeinuka na kusimama.
9BWANA, umwokoe mfalme,
Utuitikie siku tuitayo.