Zaburi 23

Zaburi 23

Mchungaji mwema

1BWANA ndiye mchungaji wangu,[#Yn 10:11; 1 Pet 2:25]

Sitapungukiwa na kitu.

2Katika malisho ya majani mabichi hunilaza,[#Ufu 7:17; Eze 34:14]

Kando ya maji ya utulivu huniongoza.

3Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza

Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.

4Naam, nijapopita kati ya bonde la kivuli cha mauti,[#Zab 46:11; Isa 8:10; Zek 8:23; Mt 1:23; Mdo 18:9,10]

Sitaogopa mabaya;

Kwa maana Wewe upo pamoja nami,

Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.

5Waandaa meza mbele yangu,

Machoni pa watesi wangu.

Umenipaka mafuta kichwani pangu,

Na kikombe changu kinafurika.

6Hakika wema na fadhili zitanifuata[#2 Kor 5:1]

Siku zote za maisha yangu;

Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Published by: Bible Society of Kenya