The chat will start when you send the first message.
1Ee BWANA, nitakuita Ewe, mwamba wangu,
Usiwe kwangu kama kiziwi.
Nisije nikafanana nao washukao shimoni,
Ikiwa umeninyamalia.
2Uisikie sauti ya dua yangu nikuombapo,
Nikipainulia patakatifu pako mikono yangu.
3Usinikokote pamoja na wasio haki,
Wala pamoja na watenda maovu.
Wawaambiao jirani zao maneno ya amani,
Lakini mioyoni mwao mna madhara.
4Uwape sawasawa na vitendo vyao,[#Ufu 22:12; 2 Tim 4:14]
Na kwa kadiri ya uovu wa matendo yao,
Uwape sawasawa na kazi ya mikono yao,
Uwalipe kile wanachostahili.
5Maana hawazifahamu kazi za BWANA,
Wala matendo ya mikono yake,
Atawavunja wala hatawajenga tena;
6Na ahimidiwe BWANA.
Maana ameisikia sauti ya dua yangu;
7BWANA ni nguvu zangu na ngao yangu.[#Zab 18:2]
Moyo wangu umemtumaini,
Nami nimesaidiwa;
Basi, moyo wangu unashangilia,
Na kwa wimbo wangu nitamshukuru.
8BWANA ni nguvu za watu wake,
Naye ni ngome ya wokovu kwa masihi wake.
9Uwaokoe watu wako, uubariki urithi wako,
Uwachunge, uwachukue milele.