The chat will start when you send the first message.
1Enyi watu wote, pigeni makofi,
Mpigieni Mungu kelele kwa Sauti ya shangwe.
2Kwa kuwa BWANA Aliye Juu, mwenye kuogofya,[#Kum 7:21; Neh 1:5; Mal 1:14]
Ndiye mfalme mkuu juu ya dunia yote.
3Amewatiisha watu wa nchi chini yetu,[#Zab 18:47]
Na mataifa chini ya miguu yetu.
4Ametuchagulia urithi wetu,[#1 Pet 1:4]
Fahari ya Yakobo ampendaye.
5Mungu amepaa kwa kelele za shangwe,[#Zab 24:7-10; Mdo 1:9; Efe 4:8-10; 1 Tim 3:16]
BWANA kwa sauti ya baragumu.
6Mwimbieni Mungu sifa, imbeni sifa;
Imbeni sifa kwa mfalme wetu, imbeni sifa.
7Maana Mungu ndiye mfalme wa dunia yote,[#Zek 14:9; 1 Kor 14:15]
Imbeni kwa zaburi.
8Mungu ayatawala mataifa,
Mungu ameketi katika kiti chake kitakatifu.
9Wakuu wa watu wamekusanyika,
Kama watu wa Mungu wa Abrahamu.
Maana ngao za dunia zina Mungu,
Ametukuka sana.