The chat will start when you send the first message.
1Mungu, unirehemu, maana yuko atakaye kunimeza,[#Zab 31:9]
Mchana kutwa ananionea akileta vita.
2Adui zangu wanataka kunimeza mchana kutwa,[#Zab 57:3]
Maana ni wengi wanaonipiga vita.
3Siku ya hofu yangu nitakutumaini Wewe;[#1 Sam 30:6; 2 Nya 20:3]
4Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake.[#Ebr 13:5,6]
Nimemtumaini Mungu, sitaogopa;
Mwenye mwili atanitenda nini?
5Mchana kutwa wanapotosha maneno yangu,
Mawazo yao yote ni juu yangu kunitakia mabaya.
6Hukutanika, hujificha, huziangalia nyayo zangu,[#Mdo 4:27,28]
Kwa kuwa waliniotea ili waniue.
7Je! Wataokoka kwa uovu wao?
Ee Mungu, uwaangamize kwa hasira yako.
8Umehesabu kutangatanga kwangu;[#Mal 3:16]
Uyatie machozi yangu katika chupa yako;
(Je! Hayamo katika kitabu chako?)
9Ndipo adui zangu watarudi nyuma siku ile niitapo.[#Isa 8:9,10]
Neno hili najua kuwa MUNGU yu upande wangu;
10Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake.
Kwa msaada wa BWANA nitalisifu neno lake.
11Nimemtumaini Mungu, sitaogopa;
Mwanadamu atanitenda nini?
12Ee Mungu, nadhiri zako ziko juu yangu;[#Zab 116:14-16]
Nitakutolea dhabihu za kushukuru.
13Maana umeniponya nafsi yangu na mauti;[#Ayu 33:30]
Je! Hukuizuia miguu yangu isianguke?
Ili niende mbele za Mungu
Katika nuru ya walio hai.