1 Wakorintho 14

1 Wakorintho 14

1UFUATIENI upendo, katakeni sana karama za rohoni, lakini zaidi mpate kukhutubu.

2Maana yeye anenae kwa lugha, haneni na watu, bali na Mungu; maana hapana asikiae; lakini anena mambo ya siri katika roho yake.

3Bali yeye akhutubuye, anena na watu maneno ya kuwajenga, na kuwafariji, na kuwatia moyo.

4Anenae kwa lugha hujijenga nafsi yake; bali akhutubuye hulijenga Kanisa.

5Nami nataka ninyi nyote mnene kwa lugha, lakini zaidi sana mpate kukhutubu; maana yeye akhutubuye ni mkuu kuliko yeye anenae kwa lugha, isipokuwa afasiri, illi kusudi Kanisa lipate kujengwa.

6Bassi, ndugu, nikija kwenu na kunena kwa lugha, nitawafaidia nini, isipokuwa nanena nanyi kwa njia ya ufunuo, au kwa njia ya elimu, au kwa njia ya khotuba, au kwa njia ya fundisho?

7Hatta vitu visivyo na uhayi vitoapo sauti, ikiwa filimbi, ikiwa kinubi, visipotoa sauti zilizo na tofauti, itatambulikanaje ni wimbo gani unaopigwa kwa filimbi au kwa kinubi?

8Kwa maana baragumu ikitoa sauti isiyojulikana, nani atakaejifanya tayari kwa vita?

9Vivyo hivyo na ninyi, msipotoa kwa ile lugha neno lililo dhahiri, neno lile linenwalo litajulikanaje? Maana nitakuwa mkinena katika hewa tu.

10Yumkini ziko sauti za namna nyingi duniani, wala hapana moja isiyo na maana.

11Bassi nisipojua maana ya ile sauti nitakuwa mshenzi kwake yeye anenae; nae atakuwa mshenzi kwangu.

12Vivyo hivyo na ninyi, kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za roho, takeni mzidi sana kuwa nazo illi kulijenga Kanisa.

13Kwa hiyo yeye anenae kwa lugha na aombe apewe kufasiri.

14Maana nikiomba kwa lugha, roho yangu huomba, lakini akili zangu hazizai matunda.

15Imekuwaje, bassi? Nitaomba kwa roho, na nitaomba kwa akili; nitaimba kwa roho, na nitaimba kwa akili.

16Kwa maana wewe ukibariki kwa roho, yeye aketiye katika daraja ya mjinga ataitikaje, Amin, baada ya kushukuru kwako, nae hayajui usemayo?

17Maana ni kweli, wewe washukuru vema, bali yule mwingine hajengwi.

18Namshukuru Mungu wangu, nanena kwa lugha zaidi ya ninyi nyote;

19lakini napenda kunena maneno matano katika kanisa kwa akili zangu, nipate kuwafundisha wengine, zaidi ya kunena maneno elfu kumi kwa lugha.

20Ndugu, msiwe watoto katika akili zenu; illakini katika uovu mwe watoto wachanga, bali katika akili zenu mwe watu wazima.

21Imeandikwa katika torati ya kama, Nitanena na watu hawa kwa watu wa lugha nyingine, na kwa midomo ya wageni, na hatta hivi hawatanisikia, asema Bwana.

22Bassi, lugha ni ishara, si kwao waaminio, bali kwao wasioamini. Lakini kukhutuhu si kwa ajili yao wasioamini, bali kwa ajili yao waaminio.

23Bassi ikiwa kanisa lote limekusanyika pamoja, na wote wananena kwa lugha, kiisha wakaingia watu wajinga au wasioamini, je! hawatasema ya kwamba mna wazimu?

24Lakini wote wakikhutubu, akaingia mtu asiyeamini, au mjinga, alaumiwa na wote, ahukumiwa na wote;

25na hivyo siri za moyo wake huwa wazi; na hivyo, akianguka kifudifudi, atamwabudu Mungu, akikiri ya kuwa Mungu yu kati yenu hila shaka.

26Imekuwaje bassi, ndugu? Mkutanapo pamoja, killa mmoja ana zaburi, ana fundisho, ana lugha, ana ufunuo, ana tafsiri. Mambo yote na yatendeke kwa kusudi la kujenga.

27Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja afasiri.

28Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa; anene na nafsi yake au na Mungu.

29Na manabii wanene wawili, au watatu, na wengine wapamhanue.

30Lakini mwingine aliyeketi, akifunuliwa neno, yule wa kwanza na anyamaze.

31Kwa maana nyote mwaweza kukhutubu mmoja mmoja, illi wote wapate kujifunza, na wote wafarijiwe.

32Na roho za manabii huwatii manabii.

33Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu.

34Wanawake wanyamaze katika kanisa, maana hawana rukhusa kunena; bali watii, kama vile inenavyo sharia nayo.

35Na wakitaka kujifunza neno, na waulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu, wanawake kunena katika kanisa.

36Je! neno la Mungu limetoka kwenu tu? au limewafikia ninyi peke yenu?

37Mtu akijiona kuwa nabii au mtu wa rohoni, na ayatambue haya ninayowaandikieni, ya kwamba ni maagizo ya Bwana.

38Lakini mtu akiwa mjinga, na awe mjinga.

39Kwa ajili ya hayo, ndugu, takeni sana kukhutubu, wala msikataze kunena kwa lugha.

40Mambo yote yatendeke kwa uzuri na kwa utaratihu.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania