1 Wakorintho 3

1 Wakorintho 3

1NA mimi, ndugu, sikuweza kunena nanyi kama na watu wenye tabia za rohoni, bali kama na watu wenye tabia za mwilini, kama na watoto wachanga katika Kristo.

2Nimewanywesha maziwa, sikuwalisha chakula; kwa maana mlikuwa hamjakiweza; naam, hatta sasa hamkiwezi, kwa maana hatta sasa m watu wa tabia za mwilini.

3Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina na faraka, je! si watu wa tabia za mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu.

4Maana hapo mtu mmoja anenapo, Mimi ni wa Paolo; na mwingine, Mimi ni wa Apolio, je! hamwi watu wa tabia za mwilini?

5Bassi Apollo ni nani? na Paolo ni nani? Ni wakhudumu ambao kwao mliamini; na killa mtu kama Bwana alivyompa.

6Mimi nilipanda, Apollo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu.

7Kama ni hivyo, apandae si kitu, wala atiae maji, bali Mungu akuzae.

8Bassi yeye apandae, na yeye atiae maji ni kitu kimoja, na killa mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe.

9Maana ninyi mwafanya kazi pamoja na Mungu: ninyi m shamba la Mungu, m jengo la Mungu.

10Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, nimeuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini killa mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake.

11Maana msingi wa namna nyingine hapana mtu awezae kuweka, illa ule uliokwisha kuwekwa, yaani Yesu Kristo.

12Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huu dhahabu au fedha au vitu vya thamani au miti au majani an manyasi,

13kazi ya killa mtu itakuwa dhahiri. Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto utajaribu kazi ya killa mtu, ni wa namna gani.

14Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu.

15Kazi ya mtu ikiteketea, atapata khasara; lakini yeye mwenyewe ataokolewa; lakini kule kuokolewa kama kwa moto.

16Hamjui ya kuwa ninyi hekalu ya Mungu, na ya kuwa Roho Mtakatifu anakaa ndani yenu?

17Kama mtu akiiharibu hekalu ya Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu ya Mungu ni takatifu, ambayo ni ninyi.

18Mtu asijidanganye nafsi yake: kama mtu akijiona kuwa mweuye hekima kati yeuu katika dunia hii, na awe mpumbavu, apate kuwa mwenye hekima.

19Maana hekima ya dunia hii ni upumbavu mbele ya Mungu. Kwa maana imeandikwa, Yeye ndiye awanasae wenye hekima katika hila yao.

20Na tena, Bwana anajua mawazo ya wenye hekima ya kwamba ni ya ubatili.

21Bassi, asijisifu mtu katika wana Adamu.

22Kwa maana vyote ni vyenu; ikiwa ni Paolo, au Apollo, au Kefa, au dunia, au uzima, au mauti, au vile vilivyo sasa, au vile vitakavyokuwa,

23vyote ni vyenu, na ninyi ni wa Kristo, na Kristo ni wa Mungu.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania