The chat will start when you send the first message.
1PAOLO, mtume wa Yesu Kristo, kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu na ya Bwana Yesu Kristo, tumaini letu;
2kwa Timotheo, mwana wangu khassa katika imani, Neema, na rehema, na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu.
3Kama vile nilivyotaka ukae katika Efeso nilipokuwa nikisafiri kwenda Makedonia, illi, nwaagize wengine wasifundishe elimu ya namna nyingine,
4wala wasiangalie hadithi na nasaba zisizo na ukomo, ziletazo maswali wala si ujenzi wa Mungu ulio katika imani; bassi sasa nakuagiza vivyo hivyo.
5Bali kusudi la mausia hayo ni upendo utokao katika moyo safi na dhamiri njema, na imani isiyo na unafiki:
6wengine wakikosa bayo wamepotea, wakigeukia maneno ya ubatili;
7wapenda kuwa waalimu wa sharia, wasiyafahamu wasemayo wala mambo yale wayanenayo kwa utbabiti.
8Lakini twajua ya kuwa sharia ni njema, kama mtu akiitumia kwa njia ya kisharia;
9nawe ufahamu neno hili, ya kuwa sharia haimkhusu mtu wa haki, bali maasi, mi wasio taratihu, na makafiri, na wenye dhambi, na wasio watakatifu, na wasiomcha Mungu, na wauao baba zao, na wauao mama zao, mi wauaji,
10na wazinzi, na wafiraji, na waibao watu, na wawongo, mi waapao uwongo, na likiwapo neno lo lote linginelo lisilopatana na mafundisho yenye uzima;
11kama vile ilivyonenwa katika injili ya utukufu wa Mungu ahimidiwae, niliyoaminiwa mimi.
12Nami namshukuru Kristo Yesu Bwana wetu aliyenitia nguvu, kwa sababu aliniona kuwa mwaminifu, akiniweka katika khuduma yake;
13mimi niliyekuwa kwanza mtukanaji, mwenye kuudhi watu, mwenye jeuri: lakini nalirehemiwa kwa kuwa nalitenda hivyo kwa njinga, na kwa kutokuwa na imani;
14na neema ya Bwana wetu ilizidi sana pamoja na imani na pendo lililo katika Kristo Yesu.
15Ni neno la kuaminiwa, listahililo kukubaliwa na watu wote, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni, awaokoe wenye dhambi; na mimi wa kwanza wao.
16Lakini kwa sababu hii nalirehemiwa, illi katika mimi, wa kwanza, Yesu Kristo adhihirishe uvumilivu wote, niwe mfano kwa wale watakaomwamini baadae, wapate uzima wa milele.
17Kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu wa hekima peke yake, kwake yeye heshima na utukufu milele na milele. Amin.
18Agizo hilo nakupa iwe akiba, mwanangu Timotheo, kwa ajili ya maneno ya unabii yalivotangulia juu yako, illi katika hayo ufanye vile vita vizuri;
19nwe mwenye imani na dhamiri njema; wengine wamezisukumia mbali hizo, wakavunja chombo cha imani.
20Katika hao wamo Humenayo na Iskander, ambao nimempa Shetani wafundishwe wasimtukane Mungu.