3 Yohana 1

3 Yohana 1

1MZEE kwa Gaio mpenzi, nimpendae katika kweli.

2Mpenzi, naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.

3Maana nalifurahi mno walipokuja ndugu na kuishuhudia kweli yako, kama nendavyo katika kweli.

4Sina furaha iliyo kuu kuliko hii, kusikia ya kwamba watoto wangu wanakwenda katika kweli.

5Mpenzi, kazi ile ni ya naminifu uwatendeayo ndugu na wageni,

6waliokushuhudia upendo wako mbele ya kanisa; utafanya vizuri ukiwasafirisha kam a ilivyo wajibu wako kwa Mungu.

7Kwa maana, kwa ajili ya Jina hilo, walitoka, wasipokee kilu kwa mataifa.

8Bassi imetupasa sisi kuwakaribisha watu kama hawo, illi tuwe watendaji wa kazi pamoja na kweli.

9Naliliandikia kanisa, lakini Diotrefe apendae kuwa wa kwanza kati yao, hatukubali.

10Kwa hiyo, nikija, nitamkumbusha matendo yake ate-ndayo, akitoa upuzi juu yetu kwa maneno maovu; wala hatoshwi na hayo, yeye mwenyewe hawakaribishi ndugu, na wale watakao kuwakaribisha, huwazuia, na kuwatoa katika kanisa.

11Mpenzi, usiuige ubaya, bali wema. Yeye atendae mema ni wa Mungu, bali yeye atendae mabaya hakumwona Mungu.

12Demetrio ameshuhudiwa na watu wote, tena na ile kweli yenyewe. Na sisi pia twashuhudu, nawe wajua ya kwamba ushuhuda wetu ni kweli.

13Nalikuwa na maneno mengi ya kukuandikia, lakini sipendi kukuandikia kwa wino na kalanm.

14Lakini nataraja kukuona karibu na kusema nawe mdomo kwa mdonm.

15Amani kwako. Rafiki zetu wakusalimu. Wasalimu rafiki, killa mtu kwa jina lake.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania