Wakolossai 1

Wakolossai 1

1PAOLO, mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo ndugu yetu,

2kwa ndugu watakatifu na waaminifu, walio ndani ya Kolossai, Neema iwe kwenu na imani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.

3Twamshukuru Mungu, baba yake Bwana wetu Yesu Kristo, siku zote tukiwaombeeni;

4tuliposikia khabari za imani yenu katika Kristo Yesu, na upendo mlio nao kwa watakatifu wote;

5kwa sababu ya tumaini mlilowekewa akiba mbinguni, khabari zake mlisikia zamani kwa neno la kweli ya Injili;

6iliyofika kwenu, kama ilivyo katika ulimwengu wote, ikizaa matunda na kukua, kama na inavyokua kwenu, tangu siku mliposikia nikaifahamu sana neema ya Mungu katika kweli;

7kama mlivyofundishwa na Epafra mjoli wetu mpenzi, aliye mkhudumu amini wa Kristo kwa ajili yenu;

8nae alitueleza upendo wenu katika Roho.

9Kwa sababu hiyo na sisi, tangu siku tuliposikia, hatuachi kuwaombeeni, na kuomba dua, mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni;

10mwenende kama ilivyo wajib wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; kwa killa kazi njema mkizaa matunda, mkizidi katika maarifa ya Mungu;

11mkiwezeshwa kwa nwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na saburi ya killa namna na uvumilivu pamoja na furaha;

12mkimshukuru Baba, aliyetustahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru;

13aliyetuokoa na uguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;

14amliae katika yeye tuna nkombozi kwa damu yake, masamaha ya dhambi,

15nae ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.

16Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya inchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni viti vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake,

17nae alikuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye.

18Nae ni kichwa cha mwili, yaani cha kanisa; nae ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, illi awe mtangulizi katika yote.

19Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae,

20na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote nae, akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya inchi, au vilivyo mbinguni.

21Na ninyi, mliokuwa hapo kwanza mmefarikishwa, ua adui katika nia zenu, kwa matendo yemi mabaya, amewapatanisha sasa,

22katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, illi awalete ninyi mbele zake, watakatifu, hamna mawaa wala lawama,

23mkidumu tu katika imani, mmewekwa juu ya misingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia khabari zake, iliyokhubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paolo nalikuwa mkhudumu wake.

24Sasa nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu; tena natimiliza yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo katika mwili wangu, kwa ajili ya mwili wake, yaani, kanisa lake,

25ambalo nimekuwa mkhudumu wake, kwa uwakili wa Mungu, niliopewa kwa faida yenu, nilitimize neno la Mungu;

26siri ile iliyofichwa tangu zamani zote na tangu vizazi vyote, bali sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake:

27ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu;

28ambae sisi tunakhubiri khabari zake, tukimwonya killa mtu, na tukimfundisha killa mtu katika hekima yote, tupate kumleta killa mtu mtimilifu katika Kristo Yesu;

29nami najitaabisha kwa hiyo, nikijitahidi kwa kadiri ya kutenda kazi kwake atendae kazi ndani yangu kwa nguvu.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania