Wakolossai 3

Wakolossai 3

1BASSI mkiwa mmefufuka panioja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu, Kristo aliko mkono wa kuume wa Mungu, ameketi.

2Nieni yaliyo juu, siyo yaliyo katika inchi.

3Kwa maana mlikufa, na uzima wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.

4Kristo atakapoonekana, aliye uzima wetu, ndipo na ninyi mtaonekana pamoja nae katika utukufu.

5Bassi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika inchi, uasharati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu:

6kwa ajili ya hayo ghadhabu ya Mungu huwafikia wana wa kuasi.

7Katika hayo na ninyi mlitembea zamani, mlipoishi katika haya.

8Lakini sasa yawekeni mbali haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na matukano, na matusi vinywani mwenu.

9Msiambiane uwongo, kwa kuwa mmemvua mtu wa kale, pamoja na matendo yake,

10mkamvaa mtu mpya anaefanywa upya apate maarifa kwa mfano wake yeye aliyemumba.

11Hapo hapana Myunani wala Myahudi, kutahiriwa wala kutokutahiriwa, mshenzi wala Mskuthi, mtumwa wala mungwana, bali Kristo ni yote, na katika wote.

12Bassi, kwa kuwa mu wateule wa Mungu, watakatifu na wapendwao, vaeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu,

13mkichukuliana, na kuachiliana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mtu; jinsi Kristo alivyowaachilieni, vivyo hivyo na ninyi.

14Juu ya haya yote vaeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.

15Na amani ya Mungu iamue mioyoni mwenu, ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; na mwe watu wa shukrani.

16Neno la Kristo likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; kwa neema mkimwimbia Bwana mioyoni mwenu.

17Na killa mfanjalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.

18Ninyi wake, watiini waume zenu, kania ipendezavyo katika Bwana.

19Ninyi waume, wapendeni wake zenu, msiwe na uchungu nao.

20Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jamlio hili lapendeza katika Bwana.

21Ninyi haha, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.

22Ninyi watumwa, watiini wao ambao kwa niwili ni bwana zenu, katika mambo yote, si kwa utumwa wa macho, kama wajipendekezao kwa wana Adamu, bali kwa unyofu wa moyo, mkimeha Mungu.

23Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wana Adamu,

24mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana njira wa urithi; kwa kuwa mnamtumikia Bwana Kristo.

25Maana adhulumuye atapata mapato ya udhalimu wake, wala hakuna upendeleo.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania