The chat will start when you send the first message.
1NINYI bwana, wapeni watumwa wenu yaliyo haki na ya adili, mkijua ya kuwa ninyi nanyi mna Bwana mbinguni.
2Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani,
3mkituombea na sisi pia, Mungu atufungulie mlango kwa Neno lake tuinene siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake nimefungwa,
4illi niidhihirishe, kama inipasavyo kunena.
5Enendeni kwa hekima mbele vao walio nje, mkiukomboa wakati.
6Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea chumvi, mpate kujua jinsi iwapasa vyo kumjibu killa mtu.
7Tukiko, ndugu mpendwa, mtumishi mwaminifu, mjoli wangu katika Bwana, atawaarifu mambo yangu yote;
8ambae nimemtuma kwenu kwa sababu hiyo hiyo, ajue mambo yenu, akawafariji mioyo yenu;
9pamoja ua Onesimo, ndugu mwaminifu, mpendwa, aliye mtu wa kwenu; watawaarifuni mambo yote ya huku.
10Aristarko, aliyefumgwa pamoja nami, awasalimu, na Marko, mjomba wake Barnaba, amhae mmepokea maagizo kwa khabari yake; akifika kwenu mkaribisheni.
11Na Yesu aitwae Yusto; hao ni watu wa tohara. Tena hao peke yao ni watendaji wa kazi pamoja nami kwa ajili ya ufalme wa Mungu; nao walikuwa faraja kwangu.
12Epafra, aliye mtu wa kwenu, mtumwa wa Yesu Kristo, awasalimu, akifanya bidii siku zote kwa ajili yenu, katika maombi yake msimame wakamilifu mkathuhutike sana katika mapenzi yote ya Mungu.
13Maana namshuhudia kwamba ana juhudi nyingi kwa ajili yenu, na kwa ajili yao walio katika Laodikia, na kwa ajili yao walio katika Hieropoli.
14Luka, yule tabibu mpendwa, awasalimu, na Dema.
15Wasalimuni ndugu walio katika Laodikia, na Numfa, na kanisa lililo katika nyumba yake.
16Waraka hun ukiisha kusomwa kwenu, fanyeni kwamba usomwe katika kanisa la Walaodikia; na ule wa Laodikia usomwe na ninyi.
17Mwambieni Arkippo, Iangalie sana khuduma ile uliyopewa katika Bwana, illi uitimize.
18Salamu yangu mimi Paolo, kwa mkono wangu mwenyewe. Yakumbukeni mafungo yangu. Neema na iwe pamoja nanyi. Amin.