Ufunuo 12

Ufunuo 12

1NA ishara kuu ilionekana mbiuguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota thenashara.

2Nae alikuwa ana mimba, akilia, akiwa ana utungu na kuumwa katika kuzaa.

3Ishara nyingine ikaonekana mbinguni; joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba.

4Na mkia wake wakokota thuluth ya nyota za mbinguni na kuziangusha katika inchi.

5Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, illi azaapo, amle mtoto wake. Akazaa mtoto mwanamume, atakaewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Na mtoto wake akanyakuliwa hatta kwa Mungu na kwa kiti cbake cha enzi.

6Yule mwanamke akakimbilia nyikani ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, illi wamlishe huku siku elfu na miateen na sittini.

7Kulikuwa na vita mbinguni: Mikael na malaika zake wakipigana na joka, joka akapigana nao pamoja na malaika zake;

8nao bawakushinda wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.

9Joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwae Msingiziaji na Shetani, audanganyae ulimwengu wote; akatupwa hatta inchi, na malaika zake wakatupwa pamoja nae.

10Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikinena, Sasa kumekuwa wokofu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake: kwa maana ametupwa mshitaki wa ndugu zetu, awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchaua na nsiku.

11Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; wala hawakupenda maisha yao hatta wakati wa kufa.

12Kwa hiyo shangilieni, mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa inchi na bahari: kwa maana yule msingiziaji ameshuka kwao mwenye hasira nyingi, akijua ya kuwa ana wakati si mwingi.

13Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika inchi alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume.

14Mwanamke yule akapewa mabawa mawili kama ya tai yule mkubwa, illi aruke, aende zake nyikani hatta mahali pake, bapo alishwapo wakati na nyakati na nussu ya wakati, mbali ya nyoka huyo.

15Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyunia ya mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule.

16Inchi ikamsaidia mwanamke, inchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake.

17Joka akamkasirikia mwanamke akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu Kristo.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania