The chat will start when you send the first message.
1NAWAPENI sifa njema za Foibe ndugu yetu, aliye mwenye khuduma katika kanisa lilioko Kenkrea,
2illi mmpokee katika Bwana, kama iwapasavyo watakatifu, mkamsaidie katika neno lo lote atakalohitaji kwenu, kwa sababu yeye nae amekuwa msaidizi wa watu wengi, akanisaidia na mimi pia.
3Nisalimieni Priska na Akula, watenda kazi pamoja nami katika Kristo Yesu,
4waliokuwa tayari hatta kukatwa kichwa kwa ajili ya maisha yangu; ambao ninawashukuru, wala si mimi tu, illa na makanisa ya mataifa yote pia;
5nisalimieni kanisa lililomo katika nyumba yao. Nisalimieni Epaineto, mpenzi wangu, aliye malimbuko ya Asia kwa Kristo.
6Nisalimieni Mariamu, aliyejitaabisha sana kwa ajili yetu.
7Nisalimieni Androniko na Junia; jamaa zangu, waliofungwa pamoja nami, walio maarufu katika mitume; nao walikuwa katika Kristo kabla yangu.
8Nisalimieni Amplia, mpenzi wangu katika Bwana.
9Nisalimieni Urbano, mtenda kazi pamoja nami katika Kristo, na Staku, mpenzi wangu.
10Nisalimieni Apelle, mwenye kukubaliwa katika Kristo. Nisalimieni watu wa nyumba ya Aristobulo.
11Nisalimieni Herodioni, jamaa yangu. Nisalimieni watu wa nyumba ya Nakisso, walio katika Kristo.
12Nisalimieni Trufina na Trufosa, wenye ijtihadi katika Kristo.
13Nisalimieni Rufo, mteule katika Kristo, na mama yake, aliye mama yangu pia.
14Nisalimieni Asunkrito, Flegoni, Herme, Patroba, Herma, na ndugu walio pamoja nao.
15Nisalimieni Filologo na Julia, Nereu na ndugu yake, na Olumpa, na watakatifu wote walio pamoja nao.
16Salimianeni kwa busu takatifu. Makanisa yote ya Kristo yawasalimu.
17Nawasihini, ndugu, waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza; mkajiepushe nao.
18Kwa sababu bao ndio wasiomtumikia Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe; na kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wasio wabaya.
19Maana utii wenu umewafikilia watu wote; bassi nafurahi kwa ajili yenu, lakini nataka mwe wenye hekima katika mambo mema, na wajinga katika mambo mabaya.
20Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu kwa upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi.
21Timotheo, mtenda kazi pamoja nami, awasalimu, na Lukio, na Yason, na Sosipatro, jamaa zangu.
22Mimi Tertio, niliyeandika waraka huu, nawasalimu katika Bwana.
23Gayo, mwenyeji wangu na wa Kanisa lote pia awasalimu. Erasto, wakili wa mji awasalimu, na Kwarto, ndugu yetu.
24Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi nyote. Amin.
25Sasa na atukuzwe yeye awezae kutufanya imara kwa injili yangu na kwa kukhubiriwa Yesu Kristo, kwa ufunuo wa ile siri iliyostirika tangu zamani za milele,
26ikadhihirishwa wakati huu kwa maandiko ya manabii, ikajulika na mataifa yote kama alivyoamuru Mungu wa milele, illi waitii imani;
27yeye ndiye Mungu mwenye hekima peke yake; na atukuzwe kwa Yesu Kristo, milele na milele. Amin.