The chat will start when you send the first message.
1WAKUMBUSHE kujinyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutii, na kuwa tayari kwa killa kazi njema,
2wasimtukane mtu, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakionyesha upole wote kwa watu wote.
3Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, maasi, tumedanganywa, tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukienenda katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana.
4Lakini wenia wa Mwokozi wetu Mungu na upendo wake kwa wana Adamu ulipoonekana,
5alituokoa, si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda, bali kwa rehema yake, kwa josho la kuzaliwa kwa pili, na kufanywa upya na Roho Mtakatifu,
6ambae alitumwagia kwa wingi kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu,
7tukifanyiziwa wema kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu.
8Neno hili ni amini, na mambo hayo nataka uyanene kwa nguvu, illi wale waliomwamini Mungu wakumbuke kudumu katika matendo mema. Haya ni mazuri, tena yana faida kwa wana Adamu.
9Maswali ya upuzi, na vitabu vya nasaba, na magomvi, na mashindano ya sharia, ujiepushe nayo. Kwa kuwa hayana faida, tena hayana maana.
10Mtu mzushi, baada ya kumwonya marra ya kwanza na marra ya pili, mkatae;
11ukijua ya kuwa mtu kama huyu amegeukia mbali, tena afanya dhambi, amejihukumu nafsi yake.
12Nitakapomtuma Artema kwako an Tukiko, jitahidi kuja kwangu hatta Nikopoli; maana huku nimekusudia kukaa wakati wa baridi.
13Zena, mjua sharia, na Apollo uwusafirishe kwa bidii; wasipungukiwe cho chote.
14Watu wetu nao wajifunze kudumu katika matendo mema kwa matumizi yaliyo lazima, illi wasiwe hawana matunda.
15Watu wote walio pamoja nami wakusalimu. Tusalimie wale watupendao katika Imani. Neema na iwe nanyi nyote. Amin.