The chat will start when you send the first message.
1Hivyo niliamua moyoni mwangu mwenyewe kuwa sitafanya safari nyingine ya huzuni kuja kwenu.
2Ikiwa nitawafanya muwe na huzuni nani atanifanya niwe na furaha? Ni ninyi tu ndiyo mnaweza kunifanya niwe na furaha. Ni ninyi ambao niliwahuzunisha.
3Naliwaandikia barua ili kwamba nijapo kwenu nisihuzunishwe na wale ambao wanapaswa kunifanya niwe na furaha. Nilijisikia kuwa na hakika ya kuwa ninyi nyote mtashiriki furaha yangu.
4Nilipowaandikia barua ya kwanza, niliiandika macho yangu yakibubujika machozi mengi. Sikuandika ili kuwafanya muwe na huzuni, bali kuwafanya mjue kwa jinsi gani ninavyowapenda.
5Mtu mmoja katika kusanyiko lenu amesababisha maumivu, ila si kwangu, bali amesababisha maumivu kwenu nyote kwa kiwango fulani. Nina maanisha amewakwaza nyote kwa namna fulani. (Sitaki ionekane kuwa mbaya sana kuliko ilivyo)
6Adhabu ambayo walio wengi miongoni mwa kusanyiko lenu walimpa inatosha.
7Lakini msameheni na kumtia moyo sasa. Hili litamsaidia asiwe na huzuni sana na asikate tamaa kabisa.
8Hivyo ninawasihi mwonesheni kuwa mnampenda.
9Hii ndiyo sababu niliandika ile barua. Nilitaka kuwapima na kuona ikiwa mna utii katika kila kitu.
10Mkimsamehe mtu, ndipo nami husamehe pia. Na kile nilichosamehe, kama nilikuwa na jambo la kusamehe, nilisamehe kwa ajili yenu. Na Kristo akithibitisha.
11Nilifanya hivi ili Shetani asipate ushindi wowote kutoka kwetu. Tunafahamu sote mipango yake ilivyo.
12Nilikwenda Troa kuwaambia watu Habari Njema juu ya Kristo. Bwana alinipa fursa ya pekee kule.
13Lakini sikuwa na amani kwa sababu sikumwona Tito pale. Hivyo niliaga na kwenda Makedonia.
14Lakini ashukuriwe Mungu ambaye siku zote hutuongoza katika gwaride la ushindi la Kristo. Mungu anatutumia sisi kueneza ufahamu juu ya Kristo kila mahali kama vile marashi yanayonukia vizuri.
15Maisha yetu ni sadaka ya harufu nzuri ya manukato ya Kristo inayotolewa kwa Mungu. Harufu nzuri ya sadaka hii huwaendea wale wanaokolewa na kwa wale wanaopotea.
16Kwao wanaopotea, marashi haya yananukia kama mauti, na huwaletea kifo. Ila kwao wanaookolewa, ina harufu nzuri ya uzima, na inawaletea afya ya uzima. Kwa hiyo ni nani aliye bora kuifanya kazi hii?
17Kwa hakika sio wale wanaozunguka wakiuuza ujumbe wa Mungu ili kupata faida! Lakini sisi hatufanyi hivyo. Kwa msaada wa Kristo tunaisema kweli ya Mungu kwa uaminifu, tukifahamu kuwa tunazungumza kwa ajili yake na mbele zake.