Ezra 10

Ezra 10

Toba ya watu

1Ezra alipokuwa anaomba na kuungama, huku akilia na kujitupa chini mbele ya nyumba ya Mungu, umati mkubwa wa Waisraeli wakiwemo wanaume, wanawake na watoto walikusanyika kumzunguka. Nao pia wakalia sana.

2Kisha Shekania mwana wa Yehieli, mmoja wa wazao wa Elamu, akamwambia Ezra, “Tumekosa uaminifu kwa Mungu wetu kwa kuoa wanawake wa kigeni kutoka mataifa yanayotuzunguka. Lakini pamoja na hili, bado liko tumaini kwa ajili ya Israeli.

3Sasa na tufanye agano mbele za Mungu wetu kuwafukuza hawa wanawake wote pamoja na watoto wao, kulingana na maonyo ya bwana wangu pamoja na wale ambao wanaogopa amri za Mungu wetu. Hili na lifanyike sawasawa na hii Sheria.

4Inuka, suala hili lipo mikononi mwako. Sisi tutaungana nawe, uwe na ujasiri ukatende hili.”

5Basi Ezra akainuka na kuwaapisha makuhani viongozi, Walawi na Waisraeli wote kufanya lile lililokuwa limependekezwa. Nao wakaapa.

6Ndipo Ezra akaondoka hapo mbele ya nyumba ya Mungu akaenda kwenye chumba cha Yehohanani mwana wa Eliashibu. Alipokuwa hapo, hakula chakula wala hakunywa maji, kwa sababu aliendelea kuomboleza kwa kuwa watu wa uhamishoni walikosa uaminifu kwa Mungu.

7Ndipo lilipotolewa tangazo Yuda yote na Yerusalemu kwa watu wote waliokuwa uhamishoni kukusanyika Yerusalemu.

8Yeyote ambaye hangejitokeza kwa muda wa siku tatu angepoteza mali yake yote, kulingana na uamuzi wa maafisa na wazee. Naye mtu huyo angefukuzwa kutoka kusanyiko la watu waliokuwa uhamishoni.

9Katika muda wa siku tatu, watu wote wa Yuda na Benyamini wakawa wamekusanyika huko Yerusalemu. Kwenye siku ya ishirini ya mwezi wa tisa, watu wote walikuwa wameketi ndani ya uwanja mbele ya nyumba ya Mungu, wakiwa na majonzi mno kwa tukio hilo na kwa sababu ya mvua kubwa.

10Ndipo Kuhani Ezra aliposimama akawaambia, “Mmekosa uaminifu, mmeoa wanawake wa kigeni, mkaongezea hatia ya Israeli.

11Sasa tubuni kwa Bwana , Mungu wa baba zenu, mkafanye mapenzi yake. Jitengeni na mataifa wanaowazunguka na wake zenu wa kigeni.”

12Kusanyiko lote wakajibu kwa sauti kubwa: “Uko sawa kabisa! Ni lazima tufanye kama unavyosema.

13Lakini hapa pana watu wengi na ni wakati wa mvua, hivyo hatuwezi kusimama nje. Hata hivyo, shauri hili haliwezi kumalizika kwa siku moja au mbili, kwa sababu tumetenda dhambi kubwa katika jambo hili.

14Maafisa wetu na watende kwa niaba ya kusanyiko lote. Kisha kila mmoja katika miji yetu ambaye ameoa mwanamke wa kigeni aje kwa wakati uliopangwa, akiwa pamoja na wazee na waamuzi wa kila mji, hadi hasira kali ya Mungu wetu katika shauri hili itakapoondolewa kwetu.”

15Yonathani mwana wa Asaheli na Yazeya mwana wa Tikwa peke yao, wakiungwa mkono na Meshulamu na Shabethai Mlawi, ndio waliopinga jambo hili.

16Basi watu wa uhamishoni wakafanya kama ilivyokuwa imependekezwa. Kuhani Ezra akachagua wanaume waliokuwa viongozi wa jamaa, mmoja kutoka kila mgawanyo wa jamaa, nao wote wakachaguliwa kwa majina. Katika siku ya kwanza ya mwezi wa kumi waliketi kuchunguza mashauri hayo.

17Katika siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza wakawa wamemaliza kushughulikia wanaume wote waliokuwa wameoa wanawake wa kigeni.

Wenye hatia ya kuoa wake wa kigeni

Kutoka wazao wa Yeshua mwana wa Yosadaki na ndugu zake:

20Kutoka wazao wa Imeri:

21Kutoka wazao wa Harimu:

22Kutoka wazao wa Pashuri:

24Kutoka waimbaji:

Kutoka mabawabu:

Kutoka wazao wa Paroshi:

26Kutoka wazao wa Elamu:

27Kutoka wazao wa Zatu:

28Kutoka uzao wa Bebai:

29Kutoka wazao wa Bani:

30Kutoka wazao wa Pahath-Moabu:

31Kutoka wazao wa Harimu:

33Kutoka wazao wa Hashumu:

34Kutoka wazao wa Bani:

38Kutoka wazao wa Binui:

43Kutoka wazao wa Nebo:

Neno: Biblia Takatifu™ Neno™ Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 na Biblica, Inc. Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote. Kiswahili Contemporary Version™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc. Used with permission. All rights reserved worldwide.
Published by: Biblica, Inc.