Hesabu 2

Hesabu 2

Mpangilio wa kambi za makabila

1Bwana aliwaambia Musa na Haruni:

2“Waisraeli watapiga kambi zao kuzunguka Hema la Kukutania kwa umbali kiasi, kila mwanaume akiwa chini ya beramu yake, pamoja na bendera ya jamaa yake.”

kambi ya makundi ya Yuda watapiga kambi chini ya beramu yao. Kiongozi wa watu wa Yuda ni Nashoni mwana wa Aminadabu.

4Kundi lake lina watu elfu sabini na nne na mia sita.

5Kabila la Isakari watapiga kambi karibu na Yuda. Kiongozi wa watu wa Isakari ni Nethaneli mwana wa Suari.

6Kundi lake lina watu elfu hamsini na nne na mia nne.

7Kabila la Zabuloni litafuata. Kiongozi wa watu wa Zabuloni ni Eliabu mwana wa Heloni.

8Kundi lake lina watu elfu hamsini na saba na mia nne.

kambi ya makundi ya Reubeni chini ya beramu yao. Kiongozi wa watu wa Reubeni ni Elisuri mwana wa Shedeuri.

11Kundi lake lina watu elfu arobaini na sita na mia tano.

12Kabila la Simeoni watapiga kambi karibu na Reubeni. Kiongozi wa watu wa Simeoni ni Shelumieli mwana wa Surishadai.

13Kundi lake lina watu elfu hamsini na tisa na mia tatu.

14Kabila la Gadi litafuata. Kiongozi wa watu wa Gadi ni Eliasafu mwana wa Deueli.

15Kundi lake lina watu elfu arobaini na tano mia sita na hamsini.

17Kisha Hema la Kukutania na kambi ya Walawi vitakuwa katikati ya kambi zote. Wao watasafiri kwa utaratibu ule ule kama walivyopiga kambi, kila mmoja mahali pake mwenyewe chini ya beramu yake.

kambi ya makundi ya Efraimu chini ya beramu yao. Kiongozi wa watu wa Efraimu ni Elishama mwana wa Amihudi.

19Kundi lake lina watu elfu arobaini na mia tano.

20Kabila la Manase litafuata baada ya Efraimu. Kiongozi wa watu wa Manase ni Gamalieli mwana wa Pedasuri.

21Kundi lake lina watu elfu thelathini na mbili na mia mbili.

22Kabila la Benyamini litafuata baada ya Manase. Kiongozi wa watu wa Benyamini ni Abidani mwana wa Gideoni.

23Kundi lake lina watu elfu thelathini na tano na mia nne.

makundi ya kambi ya Dani, chini ya beramu yao. Kiongozi wa watu wa Dani ni Ahiezeri mwana wa Amishadai.

26Kundi lake lina watu elfu sitini na mbili na mia saba.

27Kabila la Asheri watapiga kambi karibu na Dani. Kiongozi wa watu wa Asheri ni Pagieli mwana wa Okrani.

28Kundi lake lina watu elfu arobaini na moja na mia tano.

29Kabila la Naftali litafuata. Kiongozi wa watu wa Naftali ni Ahira mwana wa Enani.

30Kundi lake lina watu elfu hamsini na tatu na mia nne.

34Kwa hiyo Waisraeli wakafanya kila kitu Bwana alichomwamuru Musa. Hivyo ndivyo walivyopiga kambi chini ya beramu zao. Pia hivyo ndivyo walivyoondoka, kila mmoja akiwa na ukoo wake na jamaa yake.

Neno: Biblia Takatifu™ Neno™ Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 na Biblica, Inc. Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote. Kiswahili Contemporary Version™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc. Used with permission. All rights reserved worldwide.
Published by: Biblica, Inc.