The chat will start when you send the first message.
1Moyo wangu hauna kiburi, Ee Mwenyezi Mungu,
macho yangu hayajivuni;
sijishughulishi na mambo makuu kunizidi
wala mambo ya ajabu mno kwangu.
2Lakini nimetuliza na kunyamazisha nafsi yangu;
kama mtoto aliyeachishwa kunyonya na mama yake,
kama mtoto aliyeachishwa kunyonya
ndivyo ilivyo nafsi iliyo ndani yangu.
3Ee Israeli, mtumaini Mwenyezi Mungu
tangu sasa na hata milele.