The chat will start when you send the first message.
1Ufunuo wa Yesu Kristo aliopewa na Mungu ili awaoneshe watumishi wake mambo ambayo ni lazima yatukie hivi karibuni. Alijulisha mambo haya kwa kumtuma malaika wake kwa Yohana mtumishi wake,
2ambaye anashuhudia kuhusu kila kitu alichokiona, yaani neno la Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo.
3Amebarikiwa yeye asomaye maneno ya unabii huu, na wamebarikiwa wale wanaoyasikia na kuyatia moyoni yale yaliyoandikwa humo, kwa sababu wakati umekaribia.
Kwake yeye anayetupenda na aliyetuweka huru kutoka dhambi zetu kwa damu yake,
6na akatufanya sisi kuwa ufalme na makuhani, ili tumtumikie Mungu wake ambaye ni Baba yake. Utukufu na uwezo ni vyake milele na milele! Amen.
7“Tazama! Anakuja na mawingu,”[#1:7 Dan 7:13]
na “kila jicho litamwona,
hata wale waliomchoma”;
na makabila yote duniani
“yataomboleza kwa sababu yake.”
8“Mimi ni Alfa na Omega,” asema Bwana Mungu, “aliyeko, aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.”
9Mimi, Yohana, ndugu yenu ninayeshiriki pamoja nanyi mateso katika Yesu na katika ufalme na uvumilivu katika saburi, nilikuwa katika kisiwa cha Patmo kwa ajili ya neno la Mungu na ushuhuda wa Yesu.
10Katika Siku ya Bwana, nilikuwa katika Roho na nikasikia sauti kubwa kama ya baragumu nyuma yangu
11ikisema, “Andika kwenye kitabu haya yote unayoyaona, kisha uyapeleke kwa makanisa saba: kwa Efeso, Smirna, Pergamo, Thiatira, Sardi, Filadelfia na Laodikia.”
12Ndipo nikageuka ili nione ni sauti ya nani iliyokuwa ikisema nami. Nami nilipogeuka, nikaona vinara saba vya taa vya dhahabu,
13na katikati ya vile vinara vya taa, alikuwamo mtu kama Mwana wa Adamu, akiwa amevaa joho refu, na mkanda wa dhahabu ukiwa umefungwa kifuani mwake.[#1:13 Dan 7:13]
14Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu, nyeupe kama theluji, nayo macho yake yalikuwa kama mwali wa moto.
15Nyayo zake zilikuwa kama shaba inayongʼaa katika tanuru la moto, nayo sauti yake ilikuwa kama mngurumo wa maji mengi.
16Katika mkono wake wa kuume alishika nyota saba, na kinywani mwake ulitoka upanga mkali wenye makali kuwili. Uso wake ulikuwa kama jua likingʼaa kwa nguvu zake zote.
17Nilipomwona, nilianguka miguuni pake kama aliyekufa. Ndipo akauweka mkono wake wa kuume juu yangu na kusema: “Usiogope, Mimi ndiye wa Kwanza na wa Mwisho.
18Mimi ni Yeye Aliye Hai, niliyekuwa nimekufa, na tazama, ni hai milele na milele! Nami ninazo funguo za mauti na Kuzimu.[#1:18 Kuzimu kwa Kiyunani ni Hades , yaani mahali pa wafu.]
19“Basi andika mambo uliyoyaona, yaliyopo na yale yatakayotukia baada ya haya.
20Kuhusu siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume na vile vinara saba vya taa vya dhahabu ni hii: Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba, navyo vile vinara saba ni hayo makanisa saba.