Zaburi 43

Zaburi 43

Sala kwa Mungu wakati wa shida

1Ee Bwana, unihukumu, unitetee kwa taifa lisilo haki,[#Zab 7:8]

Uniokoe kutoka kwa mtu wa hila asiye haki.

2Kwa kuwa Wewe ndiwe Mungu uliye nguvu zangu; kwa nini umenitupa?[#Zab 28:7; Isa 26:4]

Kwa nini ninakwenda nikihuzunika, adui wakinionea?

3Nitumie nuru yako na kweli yako ziniongoze,[#Zab 2:6; 3:4]

Zinifikishe kwenye mlima wako mtakatifu na hata katika maskani yako.

4Hivyo nitakwenda madhabahuni kwa Mungu, kwa Mungu aliye

furaha yangu na shangwe yangu;

Nitakusifu kwa kinubi, Ee MUNGU, Mungu wangu.

5Nafsi yangu, kwa nini kuinama,[#Zab 42:5,11]

Na kufadhaika ndani yangu?

Umtumaini Mungu;

Maana nitamsifu tena,

Aliye msaada wangu,

Na Mungu wangu.

The Holy Bible in Kiswahili, Revised Union Version © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 2013. 
Published by: Bible Society of Tanzania