Hosea 9

Hosea 9

Furaha zimekwisha, mapatilizo yako karibu.

1Usifurahi, Isiraeli ukishangilia kama makabila mengine!

Kwani umefanya ugoni, ulipomwacha Mungu wako,

ukaupenda mshahara wa ugoni po pote, ngano zilipopurwa.

2Lakini wala purio la ngano wala kamulio la zabibu hayatawachunga,

nazo pombe zitawadanganya tu.

3Hawatakaa katika nchi ya Bwana, Efuraimu atarudi Misri,

nako Asuri watakula yenye uchafu.

4Hawatamtolea Bwana mvinyo za tambiko,

wala vipaji vyao vingine vya tambiko havitamfurahisha,

kwao wenyewe vitakuwa kama vilaji vya matanga,

wote watakaovila watajipatia uchafu,

kwani ni vilaji vyao vya kukomesha njaa tu,

haviingii Nyumbani mwa Bwana.

5Mtafanya nini, itakapokuwa siku ya mkutano au sikukuu ya Bwana?

6Kwani mtaona: waliokwenda zao kwa kukimbia maangamizo

Misri itawakusanya, namo Mofu (Memfisi) watawazika,

mapambo yao mazuri ya fedha yatatwaliwa na viwawi,

mangugi nayo yatakuwa mahemani mwao.

7Siku za mapatilizo zitafika! Siku za malipizi zitafika!

Ndipo, Waisiraeli watakapojua, kama mfumbuaji ni mpumbavu,

kama mtu wa kiroho ni mwenye wazimu,

kwani manza, ulizozikora, ni nyingi, nao upingani wako ni mwingi.

8Efuraimu ananivizia, Mungu wangu alipo,

tanzi la mtega ndege mfumbuaji huliona katika njia zake

zote,

ndio upingani uliomo nyumbani mwa mungu wake.

9Wamejitosa katika matendo mabaya kama siku zile za

Gibea;

atazikumbuka manza zao, atayapatiliza makosa yao.

10nilipomvumbua Isiraeli, alikuwa kama zabibu nyikani;

kama lilivyo tunda la limbuko la mkuyu unaoanza kuzaa,

ndivyo, baba zenu walivyokuwa nilipowaona;

lakini walipomfikia Baali-Peori,

wakajitenga kwangu, watumikie mambo yenye soni,

wakawa matapisho kama hayo mambo, waliyoyapenda.

11Utukufu wao wa Efuraimu utatoweka kwa kuruka kama

ndege,

kwa kuwa hapatakuwako atakayezaa

wala mwenye mimba wala atakayepata mimba.

12Ijapo wawakuze wana wao, na niwanyang'anye hao wana

wao,

asisalie hata mtu mmoja atakayekuwapo.

Nao wenyewe wataona mambo, nitakapoondoka kwao.

13Nilipomwona Efuraimu, alikuwa amepandwa pazuri

paelekeapo Tiro,

lakini Efuraimu naye hana budi kumtolea muuaji watoto

wake.

14Nikisema: Bwana, wape! utawapa nini?

Wape matumbo yasiyozaa na maziwa yaliyokauka!

15Ubaya wao wote ulitimia Gilgali; ndiko, nilikochukizwa

nao;

kwa huo ubaya wa matendo yao nitawafukuza Nyumbani

mwangu,

sitaendelea kuwapenda, wakuu wao wote hukataa kutii.

16Efuraimu alipopigwa, mizizi yao ikanyauka, hawatazaa tena;

ijapo wazae, nitawaua nao wapendwa wao, matumbo yao yaliowazaa.

17Mungu wangu atawatupa, kwani hawakumsikia;

ndipo, watakapokuwa wakitangatanga kwa mataifa.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania