The chat will start when you send the first message.
1Ikawa siku nyingine, wana wa Mungu walipokuja kumtokea Bwana, Satani naye akaja katikati yao kumtokea Bwana.[#Iy. 1:6.]
2Bwana akamwuliza Satani: Umetoka wapi? Satani akamjibu Bwana akisema: Natoka katika kutembea katika nchi na kujiendea huko na huko.
3Bwana akamwuliza Satani: Umemwangalia mtumishi wangu Iyobu? Kwani katika nchi hakuna mtu kama yeye, ni mnyofu wa kweli mwenye kumcha Mungu, nayo mabaya ameyaepuka, hata sasa angali anajikaza, asinikosee, ingawa umenichochea kumwangamiza bure.[#Iy. 1:1.]
4Satani akamjibu Bwana akisema: Ngozi hulipwa ngozi. Mtu huyatoa yote yaliyo yake, aiponye roho yake.
5Haya! Ukunjue mkono wako, uipige mifupa na nyama za mwili wake! Ndipo, atakapokutukana usoni pako.
6Bwana akamwambia Satani: Haya! Namtia mkononi mwako, lakini iangalie roho yake!
7Ndipo, Satani alipotoka usoni pake Bwana, akampiga Iyobu na kumwuguza majipu mabaya kutoka kwenye wayo hata utosini.
8Naye akatwaa kigae cha kujikunia, akajikalia majivuni.
9Ndipo, mkewe alipomwambia: Na sasa ungali unajikaza bado, usimkosee Mungu? Mtukane Mungu! Kisha ufe![#Iy. 19:17.]
10Akamwambia: Unasema, kama wanawake wapumbavu wanavyosema; mema tuliyapokea mikononi mwa Mungu, sasa hiki kibaya tusikipokee? Katika mambo hayo yote Iyobu hakukosa kwa midomo yake.[#Iy. 1:22; Yak. 5:11.]
11Rafiki zake Iyobu watatu walipoyasikia hayo mabaya yote yaliyompata, ndipo, walipoondoka kila mtu mahali pake, Elifazi wa Temani na Bildadi wa Sua na Sofari wa Nama, wakapatana kwenda pamoja kumpongeza na kumtuliza moyo.[#1 Mose 25:2; 36:15; Yos. 15:41; Yer. 49:7.]
12Wakayainua macho yao walipokuwa wako mbali bado, lakini hawakumtambua, wakapaza sauti zao, wakalia, wakazirarua nguo zao, kila mtu zake, wakajimwagia mavumbi kichwani na kujielekeza mbinguni.
13Wakakaa pamoja naye chini siku saba mchana kutwa na usiku kucha, hakuna aliyeweza kumwambia neno, kwani waliyaona maumivu yake kuwa makubwa mno.