The chat will start when you send the first message.
1Siku zile alitokea Yohana Mbatizaji, akapiga mbiu nyikani kwa Yudea akisema:[#Luk. 1:13.]
2Juteni! Kwani ufalme wa mbinguni umekaribia.[#Mat. 4:17.]
3Kwani huyo ndiye, aliyemtaja mfumbuaji Yesaya aliposema:
Iko sauti ya mtu apigaye mbiu nyikani:
Itengenezeni njia ya Bwana! Yanyosheni mapito yake!
4Naye Yohana alikuwa amevaa mavazi ya manyoya ya ngamia na mkanda wa ngozi kiunoni pake; chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni.[#2 Fal. 1:8.]
5Ndipo, walipomtokea wa Yerusalemu, nao wote wa Yudea na wa nchi zote za kando ya Yordani,
6wakabatizwa naye katika mto wa Yordani wakiyaungama makosa yao.
7Lakini alipoona, Mafariseo na Masadukeo wengi wakimjia, wabatizwe, akawaambia: Ninyi wana wa nyoka, nani aliwaambia ninyi ya kuwa mtayakimbia makali yatakayokuja?[#Mat. 12:34; 23:33.]
8Tendeni mazao yaliyo ya kujuta kweli!
9Msiwaze mioyoni mwenu kusema: Tunaye baba yetu, ndiye Aburahamu! Kwani nawaambiani: katika mawe haya ndimo, Mungu awezamo kumwinulia Aburahamu wana.[#Yoh. 8:33,39; Rom. 2:28-29; 4:12.]
10Miti imekwisha wekewa mashoka mashinani, kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa, utupwe motoni.[#Luk. 13:7-9.]
11Mimi nawabatiza katika maji, mpate kujuta. Lakini yeye anayekuja nyuma yangu ana nguvu kunipita mimi, nami sifai kumchukulia viatu vyake. Yeye atawabatiza katika Roho takatifu na katika moto.*[#Yoh. 1:26-27,33; Tume. 1:5.]
12Ungo wa kupepetea umo mkononi mwake, naye atapafagia pake pa kupuria ngano. Ngano zake atazikusanya, aziweke chanjani, lakini makapi atayachoma kwa moto usiozimika.[#Mat. 13:30.]
13Ndipo, Yesu alipotoka Galilea, akafika Yordani, akamjia Yohana akitaka kubatizwa naye.
14Lakini Yohana akamzuia akisema: Mimi imenipasa kubatizwa na wewe, nawe wewe unanijia mimi?
15Yesu akajibu akimwambia: Acha tu! Kwani ndivyo, inavyotupasa kuyatimiza maongozi yote. Ndipo, alipomwachia.
16Yesu alipokwisha batizwa, papo hapo, alipotoka majini, mbingu zikafunuka, akaona, Roho ya Mungu anavyoshuka kama njiwa na kumjia yeye.
17Mara sauti ikatoka mbinguni ikasema: Huyu ndiye mwanangu mpendwa, ambaye nimependezwa naye.*[#Mat. 17:5; Yes. 42:1; Ef. 1:6.]