The chat will start when you send the first message.
1Nilipoyainua macho yangu, nichungulie, mara nikaona mtu, naye alishika mkononi mwake kamba ya kupimia.[#Ez. 40:3.]
2Nikamwuliza: Unakwenda wapi? Akaniambia: Ninakwenda kuupima Yerusalemu, nione, upana wake na urefu wake ulivyo.
3Mara malaika aliyesema na mimi akatoka, kisha malaika mwingine akatokea kukutana naye,
4akamwambia: Piga mbio, umwambie yule kijana kwamba: Yerusalemu utakaa watu pasipo boma kwa wingi wa watu na nyama watakaokuwamo mwake.[#Ez. 38:11.]
5Kisha mimi nitakuwa boma la moto litakalouzunguka nao utukufu wake uliomo mwake utakuwa mimi; ndivyo, asemavyo Bwana.[#Zak. 9:8.]
6Ndivyo, asemavyo Bwana: Haya! Haya! Kimbieni, mwitoke nchi hiyo ya kaskazini! Kwani nimewatawanya ninyi katika pande zote nne za upepo wa angani; ndivyo, asemavyo Bwana.
7Haya! Jiponye, Sioni ukaaye kwake binti Babeli!
8Kwani hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Kuutokeza utukufu amenituma kwa wamizimu walioziteka mali zenu ninyi, kwani anayewagusa ninyi huigusa mboni ya jicho lake.[#5 Mose 32:10.]
9Ndipo, mtakaponiona, nikiwapungia kwa mkono wangu; ndipo, wao watakapokuwa mateka yao walio watumwa wao, mpate kujua, ya kuwa Bwana Mwenye vikosi amenituma.
10Shangilia kwa furaha, binti Sioni! Kwani utaniona, nikija kukaa katikati yako; ndivyo, asemavyo Bwana.
11Siku hiyo itakuwa, wamizimu wengi waje kuandamana na Bwana; ndipo, wao nao watakapokuwa ukoo wangu. Nitakaa katikati yako, upate kujua, ya kuwa Bwana Mwenye vikosi amenituma kwako.[#Yes. 11:10.]
12Ndipo, Bwana atakapowatwaa Wayuda, wawe fungu lake katika nchi hii takatifu, nao Yerusalemu atauchagua tena, uwe mji wake.[#Zak. 1:17.]
13Wote wenye miili ya kimtu sharti wanyamaze kimya usoni pake Bwana, kwani amekwisha kuondoka katika Kao lake takatifu![#Hab. 2:20.]