The chat will start when you send the first message.
1Basi hawa ndio watu wa mkoa, waliokwea kutoka katika ule uhamisho wa hao waliokuwa wamechukuliwa, ambao Nebukadneza, mfalme wa Babeli, aliwachukua mateka mpaka Babeli, nao wakarudi Yerusalemu na Yuda, kila mtu mjini kwake;[#Ezr 5:8; 6:2; Est 1:1; 8:9; 2 Fal 24:14-16; 2 Nya 36:20]
2ndio hawa waliokuja pamoja na Zerubabeli, Yoshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu, na Baana. Hii ndiyo hesabu ya watu wa Israeli;
3wazawa wa Paroshi, elfu mbili mia moja sabini na wawili.
4Wazawa wa Shefatia, mia tatu sabini na wawili.
5Wazawa wa Ara, mia saba sabini na watano.[#Neh 6:18]
6Wazawa wa Pahath-Moabu, wazawa wa Yeshua na Yoabu, elfu mbili mia nane na kumi na wawili.
7Wazawa wa Elamu, elfu moja mia mbili hamsini na wanne.
8Wazawa wa Zatu, mia tisa arubaini na watano.
9Wazawa wa Zakai, mia saba na sitini.
10Wazawa wa Binui, mia sita arubaini na wawili.
11Wazawa wa Bebai, mia sita ishirini na watatu.
12Wazawa wa Azgadi, elfu moja mia mbili ishirini na wawili.
13Wazawa wa Adonikamu, mia sita sitini na sita.[#Ezr 7:18; 8:13]
14Wazawa wa Bigwai, elfu mbili hamsini na sita.
15Wazawa wa Adini, mia nne hamsini na wanne.
16Wazawa wa Ateri, wazawa wa Hezekia, tisini na wanane.
17Wazawa wa Besai, mia tatu ishirini na watatu.
18Wazawa wa Harifu, mia moja na kumi na wawili.
19Wazawa wa Hashumu, mia mbili ishirini na watatu.
20Watu wa Gibari, tisini na watano.[#Yos 9:17; 2 Sam 21:2]
21Watu wa Bethlehemu, mia moja ishirini na watatu.[#Mwa 35:19; Mt 2:6; Rut 1:19; 1 Nya 2:51]
22Watu wa Netofa, hamsini na sita.
23Watu wa Anathothi, mia moja ishirini na wanane.
24Watu wa Beth-Azmawethi, arubaini na wawili.
25Watu wa Kiriath-yearimu, na Kefira, na Beerothi, mia saba arubaini na watatu.
26Watu wa Rama na Geba, mia sita ishirini na mmoja.[#Yos 18:25; 1 Sam 7:17; 15:34; Yer 31:15]
27Watu wa Mikmashi, mia moja ishirini na wawili.
28Watu wa Betheli, na Ai, mia mbili ishirini na watatu.
29Watu wa Nebo, hamsini na wawili.
30Watu wa Magbishi, mia moja hamsini na sita.
31Watu wa Elamu wa pili, elfu moja mia mbili hamsini na wanne.[#Ezr 2:7]
32Watu wa Harimu, mia tatu na ishirini.
33Watu wa Lodi, na Hadidi, na Ono, mia saba ishirini na watano.
34Watu wa Yeriko, mia tatu arubaini na watano.[#Kum 34:3; 2 Nya 28:15]
35Watu wa Senaa, elfu tatu mia sita na thelathini.
36Makuhani; wazawa wa Yedaya, wa ukoo wa Yeshua, mia tisa sabini na watatu.[#1 Nya 9:10; 24:7]
37Wazawa wa Imeri, elfu moja hamsini na wawili.[#1 Nya 24:14; Ezr 10:20]
38Wazawa wa Pashuri, elfu moja mia mbili arubaini na saba.[#1 Nya 9:12; Ezr 10:22]
39Wazawa wa Harimu, elfu moja na kumi na saba.[#1 Nya 24:8]
40Walawi; wazawa wa Yeshua, wazawa wa Kadmieli wa wawazawa wa Hodavia, sabini na wanne.[#Ezr 3:9]
41Waimbaji; wazawa wa Asafu, mia moja ishirini na wanane.
42Akina bawabu; wazawa wa Shalumu, wazawa wa Ateri, wazawa wa Talmoni, wazawa wa Akubu, wazawa wa Hatita, wazawa wa Shobai; jumla yao ni mia moja thelathini na tisa.
43Wanethini; wazawa wa Siha, wazawa wa Hasufa, wazawa wa Tabaothi;[#1 Nya 9:2; #2:43 Watumishi hekaluni waliowasaidia Walawi kazi.]
44wazawa wa Kerosi, wazawa wa Siaha, wazawa wa Padoni;
45wazawa wa Lebana, wazawa wa Hagaba, wazawa wa Akubu;
46wazawa wa Hagabu, wazawa wa Salmai, wazawa wa Hanani;
47wazawa wa Gideli, wazawa wa Gahari, wazawa wa Reaya;
48wazawa wa Resini, wazawa wa Nekoda, wazawa wa Gazamu;
49wazawa wa Uza, wazawa wa Pasea, wazawa wa Besai;
50wazawa wa Asna, wazawa wa Meunimu, wazawa wa Nefusimu;
51wazawa wa Bakbuki, wazawa wa Hakufa, wazawa wa Harhuri;
52wazawa wa Basluthi, wazawa wa Mehida, wazawa wa Harsha;
53wazawa wa Barkosi, wazawa wa Sisera, wazawa wa Tema;
54wazawa wa Nesia, wazawa wa Hatifa.
55Wazawa wa watumishi wa Sulemani; wazawa wa Sotai, wazawa wa Soferethi, wazawa wa Peruda;[#1 Fal 9:21]
56wazawa wa Yaala, wazawa wa Darkoni, wazawa wa Gideli;
57wazawa wa Shefatia, wazawa wa Hatili, wazawa wa Pokereth-Sebaimu, wazawa wa Amoni.
58Wanethini wote, pamoja na wazawa wa watumishi wa Sulemani, walikuwa mia tatu tisini na wawili.[#Yos 9:21,27; 1 Nya 9:2; Ezr 7:7; 1 Fal 9:21]
59Na hawa ndio watu waliokwea kutoka Tel-mela, na Tel-harsha, na Kerubu, na Adani, na Imeri; lakini hawakuweza kuonesha koo za baba zao, wala kizazi chao, kwamba walikuwa wa Israeli;
60wazawa wa Delaya, wazawa wa Tobia na wazawa wa Nekoda, mia sita hamsini na wawili.
61Tena wa makuhani; wazawa wa Habaya, wazawa wa Hakosi, wazawa wa Barzilai, yule aliyeoa mmojawapo wa binti Barzilai, Mgileadi, akaitwa kwa jina lao.[#1 Fal 2:7]
62Hao waliitafuta orodha yao miongoni mwa wale waliohesabiwa kwa nasaba, wasionekane; kwa hiyo walihesabiwa kuwa na unajisi.[#Hes 3:10]
63Na huyo Tirshatha akawaambia kwamba wasile katika vitu vitakatifu sana, hata atakaposimama kuhani mwenye Urimu na Thumimu.[#Neh 8:9; Law 22:2,10,15,16; Hes 18:9-11; Kut 28:30; #2:63 ni jina la heshima aliloitwa mtawala.]
64Basi hilo kusanyiko lote nzima, jumla yake ilikuwa watu elfu arubaini na mbili na mia tatu na sitini,[#Isa 10:22]
65tena, zaidi ya hao, kulikuwa na watumishi wao wa kiume na wa kike, ambao walikuwa elfu saba, na mia tatu na thelathini na saba; nao walikuwa na waimbaji wa kiume na wa kike mia mbili.
66Farasi wao walikuwa mia saba thelathini na sita; nyumbu wao, mia mbili arubaini na watano;
67ngamia wao, mia nne thelathini na watano; punda wao elfu sita, mia saba na ishirini.
68Na baadhi ya wakuu wa koo za baba zao, hapo walipoifikia nyumba ya BWANA, iliyoko Yerusalemu, walitoa mali kwa ukarimu kwa ajili ya nyumba ya Mungu, ili kuisimamisha mahali pake;[#Kut 25:2]
69wakatoa kadiri walivyoweza, na kutia katika hazina ya kazi hiyo, darkoni za dhahabu elfu sitini na moja, na mane za fedha elfu tano, na mavazi mia moja ya makuhani.[#2:69 ni sarafu, thamani yake ni kama shilingi 21.; #2:69 Mane ya fedha ni kama shilingi 136.]
70Hivyo makuhani, na Walawi, na baadhi ya watu, na waimbaji, na mabawabu, na Wanethini, wakakaa mijini mwao, naam, Israeli wote wakakaa mijini mwao.