The chat will start when you send the first message.
1BWANA, moyo wangu hauna kiburi,[#Rum 12:16]
Wala macho yangu hayainuki.
Wala sijishughulishi na mambo makuu,
Wala mambo yanayozidi nguvu zangu.
2Hakika nimeituliza nafsi yangu,[#Mt 18:3]
Na kuinyamazisha.
Kama mtoto aliyeachishwa kunyonya
Kifuani mwa mama yake;
Roho yangu ni kama mtoto,
Aliyeachishwa kunyonya.
3Ee Israeli, umtarajie BWANA,
Tangu leo na hata milele.