The chat will start when you send the first message.
1BWANA ametamalaki, amejivika adhama,[#Isa 52:7; Ufu 19:6; Ayu 40:10; Zab 104:1; Isa 59:17]
BWANA amejivika, ukuu na nguvu, kama mavazi ya kifalme.
Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike;
2Kiti chako kimekuwa thabiti tokea zamani;[#Mit 8:22]
Wewe ndiwe uliye tangu milele.
3Ee BWANA, mito imepaza,
Mito imepaza sauti zake,
Mito imepaza uvumi wake.
4Kupita sauti ya maji mengi, maji makuu,[#Zab 29:10]
Kupita mawimbi ya bahari yaumkayo,
BWANA Aliye Juu ndiye mwenye ukuu.
5Shuhuda zako ni amini sana;
Utakatifu ndio uifaao nyumba yako,
Ee BWANA, milele na milele.