The chat will start when you send the first message.
1BWANA ametamalaki, mataifa wanatetemeka;[#Kut 25:22]
Ameketi juu ya makerubi, nchi inatikisika.
2BWANA ni mkuu katika Sayuni,
Naye ametukuka juu ya mataifa yote.
3Na walisifu jina lake kuu litishalo;[#Kum 28:58; Isa 6:3; Ufu 4:8]
Ndiye mtakatifu.
4Mfalme mkuu upendaye hukumu kwa haki;[#Kum 32:3,4; Ayu 36:5; Isa 11:3-5; Yer 23:5; Mwa 18:25; #99:4 Katika Kiebrania ni nguvu za mfalme.]
Umeiimarisha haki;
Umefanya hukumu na haki katika Israeli.
5Mtukuzeni BWANA, Mungu wetu;[#1 Nya 28:2; Zab 132:7; Isa 66:1]
Sujuduni penye kiti cha miguu yake;
Ndiye mtakatifu.
6Musa na Haruni walikuwa makuhani wake,
Na Samweli pia ni miongoni mwa walioliitia jina lake,
Walimlilia BWANA naye akawaitikia;
7Akasema nao katika nguzo ya wingu.[#Kut 19:9; 33:9; Hes 12:5]
Wakashika shuhuda zake na amri aliyowapa.
8Ee BWANA, Mungu wetu, ndiwe uliyewajibu;[#Hes 14:20; Sef 3:7; Kum 9:20]
Ulikuwa kwao Mungu mwenye kusamehe
Ingawa uliwapatiliza matendo yao.
9Mtukuzeni BWANA, Mungu wetu;
Sujuduni mkiukabili mlima wake mtakatifu;
Maana BWANA, Mungu wetu, ni mtakatifu.