The chat will start when you send the first message.
1MAANA ninyi wenyewe, udugu, mwakujua kuingia kwetu kwenu, ya kwamba hakukuwa burre,
2bali tukiisha kuteswa kwanza na kutendwa jeuri, kama mjuavyo, katika Filippi, twalithubutu katika Mungu kuinena Injili ya Mungu kwenu, kwa kuishindania sana.
3Kwa maana maonyo yetu siyo ya ukosefu wala ya uchafu, wala ya hila,
4bali kama vile tulivyopata kibali kwa Mungu tuaminiwe Injili ndivyo tunenavyo; si kama wapendezao wana Adamu bali Mungu anaetupima mioyo yetu.
5Maana hatukuwa na maneno ya kujipendekeza wakati wo wote, kama mjuavyo, wala maneno ya kuficha tamaa; Muugu ni shahidi.
6Hatukutaka kusifiwa na watia Adamu, wala na ninyi, wala na wengine, tulipokuwa tuliweza kuwalemea kama mitume wa Kristo;
7bali tulikuwa wapole kati yenu, kama vile mlezi awatunzavyo watoto wake mwenyewe.
8Vivyo hivyo sisi tukiwatumaini kwa upendo mwingi, tuliona furaha kuwapeni, si Injili ya Mungu tu, bali na roho zetu pia, kwa sababu mmekuwa wapendwa wetu.
9Maana, ndugu, mnakumbuka taabu yetu na masumbufu yetu; kwa kuwa mchana na usiku tulifanya kazi tusije tukamlemea mtu wa kwenu, tukawakhubirini bivi Injili ya Mungu.
10Ninyi mashahidi, na Mungu pia, jinsi tulivyokaa kwenu ninyi mnaoamini, kwa utakatifu, na kwa haki, bila kulaumiwa;
11vile vile kama mjuavyo jinsi tulivyomwonya killa mmoja wemi kama baba amwonavyo mtoto wake, tukiwatieni moyo na kushuhudia,
12illi mwenende kama ilivyo wajib wenu kwa Mungu mwenende, awaitae muingie katika ufalme wake na utukufu wake.
13Kwa sababu hiyo sisi nasi twamshukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa mlipopokea lile neno la ujumbe la Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la kibinadamu; bali kama neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kweli kweli, litendalo kazi ndani yenu ninyi mnaoamini.
14Maana uinyi, ndugu, mlikuwa wafuasi wa makanisa ya Mungu yaliyo katika Yahudi, katika Kristo Yesu; kwa kuwa mlipata mateso yale yale kwa watu wa taifa lenu, waliyopata na hao kwa Wayahudi;
15waliomwua Bwana Yesu na manabii wao wenyewe na kutuudhi sisi, wala hawampendezi Mungu, wala hawapatani na watu wo wote;
16wakituzuia tusiseme na mataifa wapate kuokolewa; illi watimize dhambi zao siku zote; lakini hasira imewafikia hatta mwisho.
17Lakini sisi, ndugu, tukifarakana nanyi kwa kitambo, kwa nso si kwa moyo, tulitamani zaidi kuwaona nyuso zenu, kwa shauku nyingi.
18Kwa hiyo tulitaka kuja kwenu, naam, mimi Paolo, marra ya kwanza, na marra ya pili. Shelani akatuzuia.
19Maana tumnini letu, au furaha yetu, an taji ya kujisifu ni nini? Si ninyi, mbele za Bwana wetu Yesu Kristo wakati wa kuja kwake?
20Maana ninyi utukufu wetu, na furaha yetu.