The chat will start when you send the first message.
1SIMON PETRO, mtumwa na mtume wa Yesu m Kristo, kwao waiiopata imani moja na sisi, yenye thamani, katika haki ya Mungu wetu, na Mwokozi wetu Yesu Kristo.
2Neema na iwe kwenu na amani iongezwe katika kumjua Mungu na Yesu Bwana wetu;
3kwa kuwa uweza wa Mungu umetukarimia vitu vyote vyenye uzima na utawa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe;
4kwa hizo tumekarimiwa ahadi kubwa, za thamani, illi kwa hizo mpate kuwa washirika wa sifa za Mungu, mkiokolewa na ubaribifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.
5Naam, na kwa sababu hiyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenn tieni na wema, na katika wema wenu maarifa,
6na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu uvumilivu, na katika uvumilivu wenu utawa,
7na katika utawa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo.
8Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo.
9Maana yeye asiyekuwa na haya ni kipofu, hawezi kuona vitu vilivyo mbali, amesahau kule kutakaswa dhambi zake za zamani.
10Kwa hivo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara wito wenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe.
11Maana hivi mtaruzukiwa kwa ukarimu kuuingia ufalme wa milele wa Bwana wetu, Mwokozi wetu Yesu Kristo.
12Kwa hiyo sitakosa kuwakumbusheni hayo siku zote, ijapokuwa mnayajua na kuthubutishwa katika kweli iliyowatikia.
13Nami naona ni haki, maadam nipo mimi katika maskani hii, kuwaamsheni kwa kuwakumhusheni.
14Nikijua kwamba kule kuwekea mbali maskani yangu kwaja upesi, kama Bwana wetu Yesu Kristo alivyonionyesha kwa wazi.
15Walakini nitajitahidi, illi killa wakati baada ya kufariki kwangu mpate kuyakumbuka mambo haya.
16Maana hatukufuata hadithi zilozotungwa kwa werevu, tulipowajulislia ninyi nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na kuja kwake; bali tulikuwa mashahidi wa ukuu wake.
17Maana alipata kwa Mungu Baba heshima na utukufu, hapo alipoletewa sauti iliyotoka katika utukufu mkuu, ya kama, Huyu ndiye mwanangu nimpendae, amhae nimependezwa nae.
18Na santi hii ndiyo tuliyoisikia tulipokuwa pamoja uae katika mlima ule mtakatifu.
19Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ingʼaayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya assubuhi kuzuka mioyoni mwenu.
20Mkijua neno hili ya kwamba hapana unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fullani tu.
21Maana unabii haukuletwa zamani kwa mapenzi ya mwana Adamu; hali wana Adamu, watakatifu wa Mungu, walinena, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.