The chat will start when you send the first message.
1PAOLO, mtume (si mtume wa wana Adamu, wala hakutumwa na mwana Adamu, bali na Yesu Kristo, na Mungu Baba aliyemfufua),
2na ndugu wote walio pamoja nami, kwa makanisa ya Galatia,
3Neema iwe kweuu, na amani itokayo kwa Mungu Baba, na kwa Bwana Yesu Kristo,
4aliyejitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu illi atuokoe na dunia hii mbovu iliyopo sasa, kama alivyopenda Mungu, Baba yetu:
5ambae ana utukufu milele na milele, Amin.
6Nastaajabu kwa kuwa mmemwacha hivi upesi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo,
7mkageukia injili ya namna nyingine; wala si nyingine. Lakini wapo watu wawataabishao na watakao kuigeuza injili ya Kristo.
8Lakini sisi au malaika wa mbinguni tukiwakhubiri ninyi injili illa hiyo tuliyowakhubiri, na alaaniwe.
9Kama tulivyotangulia kusema, na sasa nasema tena, mtu awae yote akiwakhubiri injili illa hiyo tuliyowakhubiri, na alaaniwe.
10Maana sasa je! nawashawishi wana Adamu au Mungu? au nataka kuwapendeza wana Adamu? Kama ningekuwa hatta sasa nawapendeza wana Adamu, singekuwa mtumwa wa Kristo.
11Kwa maana injili biyo niliyowakhubiri nawajulisha, ndugu, ya kuwa siyo ya namna ya kibinadamu.
12Maana sikuipokea kwa mwana Adamu wala sikufundishwa na mtu, bali kwa ufunuo wa Yesu Kristo.
13Maana mmesikia khabari za mwenendo wangu zamani katika dini ya Kiyahudi, kwamba naliliudhi kanisa la Mungu kupita kiasi nikaliharibu,
14nami nalitangulia katika dini ya Kiyahudi kuliko wengi walio hirimu zangu katika kabila yangu, nikajitahidi sana katika kushika mapokeo ya baba zangu.
15Lakini Mungu aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake,
16alipoona vema kumdhihirisha Mwana wake ndani yangu, illi niwakhubiri mataifa khabari zake, marra sikufanya shauri na watu wenye mwili na damu,
17wala sikupanda kwenda Yerusalemi kwa hao waliokuwa mitume kabla yangu, bali nalikwenda zangu Arabuni nikarudi teua Dameski.
18Kiisha, baada ya miaka mitatu, nalipanda kwenda Yerusalemi illi nionaue na Kefa, nikakaa kwake siku kumi na tano.
19Lakini sikumwona mtume mwingine illa Yakobo ndugu yake Bwana.
20Na bayo ninayowaandikieni, angalieni, mbele za Mungu, sisemi uwongo.
21Khalafu nalikwenda pande za Sham na Kilikia.
22Lakini sikujulika uso wangu na makanisa ya Yahudi yaliyo katika Kristo;
23ilia wamesikia tu ya kwamba yeye aliyetuudhi kwanza sasa anaikhubiri imani ile aliyoiharibu zamani.
24Wakamtukuza Mungu kwa ajili yangu.