Ufunuo 1

1UFUNUO wa Yesu Kristo aliopewa na Mungu awaonyeshe watumishi wake mambo ambayo kwamba hayana buddi kuwa upesi: akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumishi wake Yohana;

2aliyeshuhudia Neno la Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo, mambo yote aliyoyaona.

3Yu kheri asomae, nao wayasikiao maneno ya unabii huu na kuyafanya yaliyoandikwa humo: maana wakati ni karibu.

4Yohana kwa makanisa saba yaliyo katika Asia: Neema iwe kwenu na amani zitokazo kwake yeye alioko na aliyekuwako nii atakaekuwako: na zitokazo kwa roho saba zilizo mbele ya kiti chake cha enzi:

5na zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi alive mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Kwake yeye aliyetupeuda na kutuosha dhambi zetu kwa damu yake,

6na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu, Baba yake: utukufu na ukuu una Yeye hatta milele na milele. Amin.

7Tazama yuaja na mawingu: na killa jicho litamwona, na hawo waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amin.

8Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisiio, asema Bwana Mungu, alioko, aliyekuwako, na atakaekuwako, Mwenyiezi.

9Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na uvumilivu wa Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu.

10Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu,

11ikinena, Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho. Haya uonayo yaandike katika chuo, ukayapeleke kwa makanisa saba yaliyo katika Asia; Efeso, na Smurna, na Pergamo, na Thuatera, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.

12Nikageuka niione ile sauti iliyosema nami. Na nilipogeuka, nikaona vinara saba vya dhahabu;

13na kati kati ya vile vinara nikaona mtu kwa mfano wa Mwana Adamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini.

14Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama thuluji; na macho yake kama mwako wa moto:

15na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji mengi.

16Nae alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume: na upanga mkali, mkali kuwili, watoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua likingʼaa kwa nguvu zake.

17Na nilipomwona nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akiniambia, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,

18na aliye hayi; nami nalikuwa nimekufa, na tazama ni hayi hatta milele na milele. Amin. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.

19Bassi, yaandike mambo uliyoyaona, nayo yatakayokuwa baada ya hayo.

20Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhababu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba, na vile vinara saba ulivyoviona ni makanisa saba.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania