The chat will start when you send the first message.
1Hii itakuwa ni safari yangu ya tatu kuwatembelea. Na mkumbuke, “Kila shitaka ni lazima lithibitishwe na mashahidi wawili au watatu wanaosema kuwa jambo hilo ni la kweli.”[#Kum 19:15]
2Nilipokuwa pamoja nanyi mara ya pili, nilitoa maonyo kwa wale waliotenda dhambi. Sipo hapo sasa, ila natoa onyo lingine kwao na kwa yeyote aliyetenda dhambi: Nitakapo kuja tena kwenu, nitawaadhibu walio miongoni mwenu ambao bado wanatenda dhambi.
3Mnatafuta uthibitisho kuwa Kristo anasema kupitia mimi. Uthibitisho wangu ni kuwa yeye si dhaifu kuwashughulikia bali yeye anaonesha uweza wake miongoni mwenu.
4Ni kweli kuwa Kristo alikuwa dhaifu alipouawa msalabani, lakini yu hai kwa nguvu za Mungu. Ni kweli pia kwamba twashiriki unyonge wake, lakini kwa kushughulika nanyi, tutakuwa hai pamoja nae katika uweza wa Mungu.
5Jiangalieni ninyi wenyewe. Mjipime ninyi wenyewe mkaone kama mngali mnaishi katika imani. Hamtambui kuwa Kristo Yesu yu ndani yenu? La mkishindwa jaribio hilo; ikiwa hamtakuwa mkiishi katika imani; basi Kristo hayumo ndani yenu.
6Lakini ni matumaini yangu kuwa mtagundua ya kwamba hatujashindwa jaribio hilo.
7Tunawaombea kwa Mungu msifanye lolote lililo baya. Tunachojali hapa si kwamba watu waone kuwa tumeshinda jaribio katika ile kazi tuliyofanya pamoja nanyi. Tunachokitaka zaidi ni ninyi kufanya lililo jema, hata ikiwa itaonekana kuwa tumeshindwa jaribio.
8Hatuwezi kufanya lolote lililo kinyume na kweli bali lile linalodumisha kweli.
9Tunafuraha kuonekana tu wadhaifu ikiwa ninyi mko imara. Na hili ndilo tunaloomba, kwamba maisha yenu yatakamilishwa katika haki tena.
10Ninaandika haya kabla sijaja kwa kuwa niko mbali nanyi ili nijapo nisilazimike kutumia mamlaka kuwaadhibu. Bwana alinipa mamlaka hayo kuwaimarisha, na sio kuwaharibu.
11Sasa, wapendwa dada zangu na kaka zangu mjazwe furaha. Jitahidini kutengeneza njia zenu, fanyeni nilichowaomba kufanya. Mpatane kila mmoja na mwenziwe, na ishini katika amani. Ndipo Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.
12Msalimiane kwa salamu maalum ya watu wa Mungu. Watakatifu wote wa Mungu hapa nao wanawasalimu.[#13:12 Kwa maana ya kawaida, “busu takatifu”.]
13Ninawaombea ili ninyi nyote mfurahie neema ya Bwana Yesu Kristo, upendo wa Mungu, na Ushirika wa Roho Mtakatifu.[#13:13 Hii inaweza kumaanisha kushirikiana katika Roho Mtakatifu au kupenda kushirikishana mambo na kukaa katika umoja wa waamini kunakofanywa na Roho Mtakatifu.]