2 Timotheo 2

2 Timotheo 2

Askari Mwaminifu wa Kristo Yesu

1Kwako wewe mwanangu, uwe hodari kwa njia ya neema inayopatikana kwa Kristo Yesu.

2Yachukue mambo uliyoyasikia kwangu mbele za mashahidi wengi, na yakabidhi kwa watu waaminifu ambao watakuwa na uwezo wa kuwafundisha wengine pia.

3Kama askari mwaminifu wa Kristo Yesu, jiunge nami katika mateso.

4Hakuna hata mmoja anayefanya kazi kama askari kisha akajishughulisha pia na mambo ya kiraia. Hii ni wa sababu anataka kumfurahisha kamanda wake.

5Na kama kuna mtu anayeshiriki katika mashindano ya riadha, hawezi kushinda taji endapo hatashindana kwa kufuata sheria.

6Mkulima mwenye juhudi anastahili kuwa wa kwanza kufurahia sehemu ya mavuno yake.

7Nakutaka wewe kuyafikiri ninayokuambia na Bwana atakupa uwezo wa kuyaelewa mambo haya yote.

8Endelea kumkumbuka Yesu Kristo, aliyefufuka kutoka kwa wafu, na ni kutoka ukoo wa Daudi. Na huu ndiyo Habari Njema ninayoihubiri.

9Kwa sababu ya Habari Njema ninateseka, hadi hatua ya kufungwa kwa minyororo kama mhalifu. Lakini ujumbe wa Mungu haujafungwa.

10Kwa hiyo nayavumilia yote kwa ajili ya wateule wa Mungu, ili na wao waweze kuufikia wokovu unaopatikana katika Kristo Yesu, pamoja na utukufu wa milele.

11Na hapa kuna usemi wa kuaminiwa:

Kama tumekufa pamoja naye,

tutaweza kuishi naye pia.

12Kama tutastahimili, tutaweza pia kumiliki pamoja naye.

Kama tutamkana yeye, naye atatukana sisi.

13Kama hatutakuwa waaminifu,

yeye anabaki kuwa mwaminifu,

kwa sababu hawezi kujikana mwenyewe.

Mtendakazi Ampendezaye Mungu

14Endelea kuwakumbusha watu juu ya mambo haya. Waonye kwa mamlaka mbele za Mungu wasipigane juu ya maneno. Mapigano hayo hayana mambo mazuri, bali huwaharibu wanaoyasikiliza.

15Jitahidi kujionesha mwenyewe kuwa umekubaliwa na Mungu, kama mtumishi asiye na kitu cho chote cha kumfadhaisha na anayeufanyia kazi ujumbe wa kweli ya Mungu katika njia sahihi.

16Bali uyaepuke majadiliano ya kijinga ya kidunia, ambayo huwapeleka watu mbali na Mungu,

17na mafundisho ya wale wanaoyachukua mafundisho hayo wanaenea kama saratani mwilini. Miongoni mwao wamo Himenayo na Fileto,

18aliyeiasi na kuikosa kweli. Wanasema kuwa ufufuo kutoka kwa wafu kwa watu wote umekwisha kutokea, na wanageuza imani za watu wengine.

19Hata hivyo, msingi ulio imara ambao Mungu aliuweka unasimama imara, na maneno haya yameandikwa juu yake: “Bwana anawajua wale walio wake,” na “Kila anayesema kuwa ni wa Bwana aweze kuuacha ubaya.”[#Hes 16:5]

20Ndani ya nyumba kubwa hakuna vyombo vya dhahabu na fedha pekee, bali hata vya udongo na mbao. Na vingine ni vya kutumika kwa matukio maalumu, na vingine ni kwa matumizi ya kawaida.

21Hivyo mtu akitakaswa kutoka maovu yote, atakuwa mtakatifu na chombo maalumu cha kutumiwa na Bwana kilicho tayari kwa kila kazi njema.

22Bali uzikimbie tamaa za ujana na kuyatafuta maisha ya haki, imani, upendo na amani, pamoja na wote wanaomwita Bwana kwa mioyo safi.

23Nyakati zote ujiepushe na mabishano ya kijinga, kwa sababu unajua kuwa huleta mabishano makubwa.

24Kwani mtumwa wa Bwana hapaswi kubishana, bali kuwa mkarimu kwa watu wote, mwenye ujuzi katika kufundisha na asiye mtukanaji.

25Anapaswa kuwaelekeza wapinzani wake kwa upole katika tumaini kwamba Mungu anaweza kuwasaidia hao kutubu na kuujua ukweli,

26na ili waweze kurudi katika fahamu zao na kuuepuka mtego wa adui, ambako wameshikiliwa kama mateka na Ibilisi na wamelazimishwa kuyafanya mapenzi yake.

Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi Toleo la Awali © 2017 Bible League International
Published by: Bible League International