The chat will start when you send the first message.
1Mwenyezi-Mungu amwambia bwana wangu:[#Taz Mat 22:44; Marko 12:36; Luka 20:42:43; Mate 2:34-35; 1Kor 15:25;]
“Keti upande wangu wa kulia,
hata niwaweke maadui zako chini ya miguu yako.”
2Mwenyezi-Mungu ataeneza enzi yako kutoka Siyoni;
utatawala juu ya maadui zako wote.
3Watu wako watakujia kwa hiari,
siku utakapokwenda kuwapiga maadui.
Juu ya milima mitakatifu watakujia vijana wako,
kama umande unaotokeza alfajiri mapema.
4Mwenyezi-Mungu amekuapia wala hatabadili nia yake:[#Taz Ebr 5:6; 6:20; 7:17,21]
“Wewe ni kuhani milele kwa utaratibu wa ukuhani wa Melkisedeki.”
5Bwana yuko upande wako wa kulia;
atawaponda wafalme atakapokasirika.
6Atayahukumu mataifa na kuwaua watu wengi;
atawaponda viongozi kila mahali duniani.
7Mfalme atakunywa maji ya kijito njiani;
naye atainua kichwa juu kwa ushindi.