Zaburi 121

Zaburi 121

Mungu kinga yetu

1Natazama juu milimani;

msaada wangu utatoka wapi?

2Msaada wangu watoka kwa Mwenyezi-Mungu,

aliyeumba mbingu na dunia.

3Hatakuacha uanguke;

mlinzi wako hasinzii.

4Kweli mlinzi wa Israeli

hasinzii wala halali.

5Mwenyezi-Mungu ni mlinzi wako;

yuko upande wako wa kulia kukukinga.

6Mchana jua halitakuumiza,

wala mwezi wakati wa usiku.

7Mwenyezi-Mungu atakukinga na baya lolote;

atayalinda salama maisha yako.

8Mwenyezi-Mungu atakulinda katika shughuli zako zote[#121:8 Kiebrania: Uingiapo na utokapo, kwa maana ya jumla, popote uendapo au ulipo.]

tangu sasa na hata milele.

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (Yenye Vitabu vya Deuterokanoni): Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa (BHN): Hakimiliki -1995, 2001: kwa Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania