The chat will start when you send the first message.
1Ee Mungu, umetutupa na kutuponda,
umewaka hasira, tafadhali uturudishie nguvu.
2Umeitetemesha nchi na kuipasua;
uzibe nyufa zake kwani inabomoka.
3Umewatwika watu wako mateso;
tunayumbayumba kama waliolewa divai.
4Uwape ishara wale wanaokuheshimu,
wapate kuuepa mshale.
5Uwasalimishe hao watu uwapendao;
utuokoe kwa mkono wako, na kutusikiliza.
6Mungu amesema kutoka patakatifu pake
“Sasa nitaigawa Shekemu kwa shangwe,
Bonde la Sukothi nitalipima sehemusehemu.
7Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu;
Efraimu ni kofia yangu ya chuma,
na Yuda ni fimbo yangu ya enzi.
8Moabu ni kama bakuli langu la kunawia,
kiatu changu nitaitupia Edomu kuimiliki.
Nitapiga kelele ya ushindi juu ya Filistia.”
9Ni nani atakayenipeleka kwenye mji wa ngome?
Ni nani atakayeniongoza mpaka Edomu?
10Je, umetuacha kabisa, ee Mungu?
Wewe huendi tena na majeshi yetu!
11Utupatie msaada dhidi ya maadui zetu,
maana msaada wa binadamu haufai kitu.
12Mungu akiwa upande wetu tutashinda,
yeye atawaponda maadui zetu.